Advertisements

Friday, November 20, 2015

Dk Tulia ajiangalie mambo matano

By Frank Sanga, Mwananchi

Dk Tulia Ackson amechaguliwa kuwa naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hiyo ni baada ya kumshinda mpinzani wake kutoka chama cha CUF, Magdalena Sakaya.

Hata hivyo, licha ya kupata ushindi huo, kuna mambo matano ambayo Dk Tulia anapaswa kujirekebisha na hasa atakapokuwa akiliongoza Bunge hilo.

Kwanza, anatakiwa kujiamini. Jana wakati akiomba kura kwa wabunge, Dk Tulia alionekana kutojiamini kiasi kwamba hata hotuba yake ya dakika tatu tu alizopewa alikuwa akiisoma. Unapopata dakika chache kama hizo unatakiwa kuonyesha umahiri wako, hasa ikizingatiwa kuwa alijua mapema kwamba angekwenda kuomba kura kwa wabunge.

Lakini pia, wakati akijibu maswali alionekana kutojiamini zaidi kwa sababu badala ya kujibu maswali, alitaka kutoa maelezo marefu jambo ambalo lilifanya ashindwe kujibu maswali mawili na kuruhusiwa kuondoka kutokana na kelele za wabunge wa upinzani.

Pili, awe mtulivu zaidi kama jina lake. Unapokuwa na nafasi kama ya naibu spika unatakiwa kuwa mtulivu. Lakini wakati akiomba kura na wakati wa maswali kutoka kwa wabunge, Dk Tulia hakuwa ametulia na alionekana kama hakujiandaa. Atakapokuwa analiongoza Bunge anatakiwa kutulia zaidi na asikubali kuyumbishwa.

Tatu, asipende mapambano. Unapokuwa naibu spika unatakiwa kusikiliza pande zote mbili, wapinzani na chama tawala. Kosa kubwa ambalo hufanywa na viongozi wetu ni kujaribu kupambana. Wakati akijieleza na wakati wa maswali, wabunge wa upinzani walikuwa wakimchokoza, ndipo Dk Tulia alipotaka kupambana kwa kutaka kujibizana nao na kama si busara za Spika Job Ndugai kuingilia kati na kumruhusu aondoke, huenda angesababisha mabishano makubwa.

Unapokuwa sehemu kama hiyo unatakiwa kuwashawishi wabunge wakusikilize na si kupambana nao.

Nne, awe na maelezo mafupi. Kwa mazingira ya sasa ya Bunge letu ambalo limejaa ushabiki zaidi wa kivyama, Dk Tulia anapaswa kujua kuwa maelezo marefu yanaweza kusababisha kutoka nje ya mstari na kuibua maswali kwa upande mmojawapo. Ni vizuri kujikita katika majibu ya moja kwa moja kuliko kutoa maelezo ambayo pengine hayawezi kusaidia sana.

Tano, asidhani anaowaongoza ni mbumbumbu. Kwa kiwango chake cha elimu na nafasi alizowahi kushika, hapana shaka kuwa Dk Tulia ni mjuzi na mbobezi. Hata hivyo, ajue kuwa aliowashinda pia wamebobea katika masuala ya kanuni za Bunge na sheria za nchi ila yeye amepata fursa. Nilipokuwa nikifuatilia majibu ya Dk Tulia kutokana na maswali ya wabunge, niligundua alikuwa akitaka kujionyesha kuwa yeye si mtu wa mchezo.

Alidhani maswali anayoulizwa ni ya mtego, hivyo akataka kuonyesha umahiri kwa kutoa maelezo yasiyohitajika. Katika nafasi ya uongozi kuna majaribu mengi, hizo ni changamoto za kawaida, lakini akijaribu kudhani anaowaongoza hawajui atajiweka katika matatizo wakati wote katika Bunge lenye mihemko ya kisiasa. Kwa ujumla, hakuna mtu ambaye anaweza kujisifu kuwa anaweza kuliko mtu mwingine. Dk Tulia amepata fursa kuonyesha uwezo wake na jambo la muhimu apewe muda tu. Namtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya.

7 comments:

Unknown said...

Jina la naibu spika ni Dkt. Tulia Ackson Mwansasu.

Kumuita Dkt. Tulia ni kumkosea heshima. Ama umuite Tulia tu kama mnafahamiana kihivyo au umuite ipaswavyo kwa wasifu wake, yani:

Dkt. Tulia Ackson Mwansasu
Dkt. Mwansasu
Dkt. Ackson

Kufuatilia mapenzi yake mwenyewe. Haipendezi kumuita Dkt. Tulia. Ni kama kumdharau hivi.

Sijaona popote pale waandishi wanapomuita:

Raisi Magufuli kama Dkt. John au
Raisi Kikwete kama Dkt. Jakaya au
Mzee Mengi kama Dkt. Reginald

Kwa nini tunamkata jina huyu mama na kumuita Dkt. Tulia?

Anonymous said...

Hapo unaposema asitoe maelezo marefu unakosa.maana kuna wengine hawajui mambo hvyo wanatakiwa wapewe maelezo ili asiruhusu sali nyingine.maana unavyomueleza mtu ka urefu na kama kuna mwingine alikuwa na sali basi lijijibu humo.Sema tu alikosa kujiamini hilo naweza kukubaliana na ww.Na pia yeye si mzoefu sana wa bungeni hvyo na imani akizoea atapata kujiamini.na maswali alijibu vizuri.Sema wapinzani hawakuwa na subira ya kusikiliza na matokeo yake wakawa wanafanya ushabiki na wametunyima kujua mambo muhimu sisi wananchi wengine.Jibu la tatu ambalo alikuwa analijibu lilikuwa muhimu kwa kila mtanzania kutambua nani anaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama fulani na kwa wakati gani na nai hapasi kabisa kushiriki mchakato wa kuingia ndni ya chama.Maoni yangu upinzani wawe na heshima ndani ya bunge hata kama mtu hamumtaki.Wanatukosesha haki sisi wananchi ya kujua vitu vingi wakati wao wanapopiga makelele.Binafsi wameniudhi.

Anonymous said...

Kwenye msafara wa mamba hata kenge wamo! Sio kila anayeandika habari ni journalist, in the strictest sense of the word! Obviously, writing skills za huyu mwandishi ziko chini ya kiwango cha hata amateurish journalism.

Anonymous said...

This Is all bullshit from Mr Sanga. There are just too many men willing to bring down women rather than acknowledging their capabilities and intellectual acumen. Eti hajiamini! I bet the Deputy Speaker is just too intelligent for the likes of Mr Sanga. Shame on him.

Anonymous said...

Watanzania ujinga utatutoka lini. Huyu dada kuitwa Dkt Tulia kunampunguzia nini....mbona Rais Yoweri Kaguta Mseveni anaitwa Mseveni na hakuna anayelalamika. Acheni hayo mambo ya kujikweza.ndiyo maana Mwalimu Julius Kambarage nyerere alikataa kuitwa muheshimiwa. Jina la Dkt Tulia alipewa na wazazi wake.

Anonymous said...

Watanzania inabidi tuwe na subira mpeni nafasi ya kujenga confidence mwenyewe, kwani aliowafundisha kazi ya uspika akina Anna Makinda, Ndugai wasiokuwa hata na profession ya law ni akina nani.Give her a room please!

Anonymous said...

Pumba juu ya pumba!