Advertisements

Sunday, November 1, 2015

IBADA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU GODFREY MNGODO COLUMBUS, OHIO

Pr. Mwakabonga akiongoza ibada ya kumbukumbu ya marehemu Godfrey Mbiu Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekani na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wafanyakazi wa kituo cha utangazaji Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili (VOA). Marehemu Godfrey Mbiu Mngodo aliaga Dunia Tarehe 11 Septemba, 2015 Dar es Salaam na kuzikwa Tanga. Godfrey Mbiu Mngodo amefanya kazi katika sehemu mbalimbali kama Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Voice of America, wizarani na kituo cha Channel Ten ameacha watoto 10 na wajukuu 14. picha na Vijimambo/ Kwanza Production
Mmoja ya mtoto wa marehemu Michael Mngodo akiwa na mwanae Alvin wakifuatilia ibada ya kumbukumbu ya mpendwa baba yake marehemu Godfrey Mbiu Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekani.
Familia ya Mngodo ikifuatilia Ibada.
Pr. Mwakabonga akifanya maombi kwa wanafamilia.
Michael Mngodo akisoma wasifu wa mpendwa baba yake. Kulia ni mtoto wake Alvin.
Ndugu, jamaa na marafiki wakifuatilia ibada. Kwa picha zaidi Bofya soma zaidi

4 comments:

Anonymous said...

Poleni sana. Hivi marehemu alikuwa baba wa the late Hilda Ngodo?( RIP).

Chemi Che-Mponda said...

Poleni sana. Sikuwa na habari kuhusu Ibada, ningehudhuria. Mzee Mngodo alikuwa mwalimu wa TSJ na pia alikuwa rafiki wa marehemu baba yangu tangu miaka ya 1960's. Rest in peace Mzee Mngodo.

Anonymous said...

Alikuwa Baba mdogo wa Hilda Mngodo.

Anonymous said...

Baba ametuonyesha picha za marehemu baba yako, naamini alikuwa ni Alec Che-Mponda. Wakiwa wote miaka hiyo ya 1960...RIP baba yetu, rafiki yetu.