
Edward Lowassa, amehoji maswali matatu kwa Rais Dk. John Magufuli.Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, Lowassa amemtaka Rais Magufuli baada ya kusema hakuna mtoto atakayelipa ada kuanzia Januari, mwakani, atamke mustakabali wa wanafunzi walioko shuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.
Lowassa amesema kwa upande wake ahadi ya elimu bure aliyokuwa akiinadi wakati wa kampeni, ilikuwa ni kuanzia shule ya awali hadi chuo kikuu na kwamba hata wale walioko mashuleni, wangeguswa na hatua hiyo.
“Niliahidi watoto wote walioko na watakaoanza shule kuanzia kindergarten (shule ya awali) hadi chuo kikuu, serikali yetu ingegharimia. Na nilitangaza kufuta michango yote shuleni ili kumpunguzia mzigo mwananchi,” alisisitiza Lowassa ambaye amekataa kuyatambua matokeo ya ushindi wa Dk. Magufuli akidai kuwa yeye ndiye aliyeshinda kwa asilimia 62 ya kura zote zilizopigwa.
Kuhusu suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, Lowassa amesema yeye alishaweka wazi kuwa elimu ingekuwa bure hadi chuo kikuu.
“Vijana hawa wanahangaika na mikopo na nasikia ni asilimia 17 tu kati ya wanafunzi 70,000 ndiyo waliopata mikopo. Sera ya Chadema na Ukawa kwa ujumla, ni kufuta kabisa shida hizi kwa serikali kufadhili elimu yao,” alifafanua Lowassa katika taarifa yake hiyo. Kwa msingi huo, Ukawa kupitia kwa aliyekuwa mgombea wao wa urais, Lowassa, umewataka wananchi kutofautisha ahadi ya elimu bure iliyotolewa na Rais Magufuli na ile iliyotolewa na Ukawa.
Lowassa alisema Magufuli ametoa maelekezo kwa watendaji wa serikali kuweka mikakati ya kutekeleza ahadi yake kuanzia Januari, mwakani kwamba hakuna mtoto atakayelipa ada.
Hata hivyo, amesema hajaeleza waziwazi hatma ya wanafunzi walioko mashuleni kama wataguswa na hatua hiyo au la.
CHANZO: NIPASHE
7 comments:
huyu Lowasssa ana haraka ya nini kujua mipango ya Mheshimiwa Pombe, kama yeye ilikuwa ni moja ya policy zake akishinda, ajue sasa yeye kashindwa na watu hawakumwelewa policy zake, asubiri mipango moto moto ya Mheshimiwa, mi nafikiri kwasababu alijiona kashinda hata akili yake kujirudi kuwa kashindwa imekuwa ni ngumu, Pole Lowassa umeshindwa tulia wacha watu wafanye kazi, mbele kwa mbele!!!!
mashindano au?swala atekeleze alichosema na sio kuiga cha wengine
Wewe Lowassa unazungumza na nani na huku humtambui Rais Magufuli? Nyamaza, na uende kimya kuchunga ng'ombe Monduli; ng'ombe wako wanakulilia!
Kuwa mpole mzee, muda wa ushindani umekwisha fanya shughuli zako kwa amani na utulivu ya nini malumbano!!!!!!!!!!!!!
Wadau, mimi nilisema toka awali kwamba huyu jamaa aende kupata tiba za kichwa, he is insane, period. He fails to understand that voters rejected his proposals at the ballot box. Technically, he is irrelevant policy-wise. kwa nini anajisumbua kufungua mdomo, wakati aliahidi kuwa ataenda kuchunga ng'ombe zake? P'se, do us a favor and just shut-up, Tanzania is moving forward without you.
yaani ananikera kila mtu alietangaza sera zake ana jinsi ya kuzitekeleza sasa huyu sijui kakurupukia wapi. hajazoea kukaa bila uongozi hili ndio tatizo tunamuomba aongoze na kuwapa amri hao ngombe sio tingatinga anajua kilichompeleka ikulu
hayo masuala ungeweza kuyaweka bayana wakati wa kampeini. Lkini ulikuwa ukichukua dakika chini ya 15 kuzungumza utumbo tu!
Post a Comment