Ofisa Uhusiano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rosemary Malale, alisema orodha hiyo ya wageni walioalikwa, inajumuisha mashirika ya kimataifa, mashirika ya kikanda, wakuu nchi na mabalozi.
Rais mteule Dk Magufuli alitangazwa kuwa mshindi, baada ya kushinda katika uchaguzi, uliofanyika wiki iliyopita kwa kupata asilimia 58.46 ya kura zote zilizopigwa. Ofisa huyo alisema wizara pia imetuma mialiko kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), inayoundwa na Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Nchi nyingine zilizoalikwa ni za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Afrika (AU).
Aidha, sherehe hizo pia zinatarajiwa kuhudhuriwa na Muungano wa nchi za Amerika (ISSR), Misri, Ghana, Sweden, Uingereza, Marekani, Ufaransa, Japan, China na Umoja wa Mataifa.
Maandalizi ya sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam yanaendelea, yakihusisha wanajeshi ambao pamoja na mazoezi mbalimbali, pia zilionekana ndege za kivita angani.
Dk Magufuli aliwaangusha wagombea wengine saba, akiwemo mpinzani wake mkuu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.
Wakati rais huyo mteule akisubiri kuapishwa, kumekuwa na ushauri tofauti kutoka kwa watu wa kada mbalimbali, wakitaka atekeleze ahadi zake na pia kujenga umoja wa Watanzania.
Akizungumza jana na mwandishi wa habari hizi, mmoja wa waliogombea urais, MacMillan Lyimo (TLP), alisema alimtaka Magufuli akiingia madarakani, ahakikishe anajenga umoja miongoni mwa Watanzania kwa kuepuka kujenga chama chake pekee.
HABARI LEO
3 comments:
KARIBUNI WANA CCM [WANANCHI WENGI HAMTATUONA NG'O],KARIBUNI WAGENI WETU WA KIMATAIFA MULIOALIKWA KWA GHARAMA ZA SERIKALI YA TANZANIA ILI MJE KUSHUHUDIA RAIS MTEULE WA AWAMU YA TANO MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI ANAAPISHWA.KARIBUNI UWANJA WA TAIFA ULIYOPO WILAYA YA TEMEKE,NGOME MPYA YA MUUNGANO WA VYAMA VYA UPINZANI TANZANIA [UKAWA].MADIWANI WENGI HAPA NI UKAWA,MBUNGE MTEULE NI UKAWA,MEYA WA MANISPAA YA TEMEKE ATAKUWA NI UKAWA.YAANI HAPA,UKAWA NDIYO KIILA KITU.MNAKUJA LEO WANA CCM KWA KUJIBANZA-BANZA,POLENI.TEMEKE NI NGOME MPYA IMARA YA UKAWA ASANTE MUNGU.SALAMU ZINAENDELEA.KUWEPO KWENU WAGENI WETU NI KWAMBA MMEPIGWA CHANGA LA MACHO, KUJA KUSHUHUDIA ALIYEPITISHWA NA TUME TA TAIFA YA UCHAGUZI WAKATI MSHINDI HALALI WA WAPIGA KURA NI MHESHMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA.MWISHO,WAGENI WETU,OMBI.MSIONDOKE TANZANIA BILA KUMTEMBELEA NA KUMUONA,MHE.LOWASSA.MKIMTEMBELEA MUMEUONA MLIMA KILIMANJARO-MNAJUA MAANA YAKE?-KARIBUNI TEMEKE YA UKAWA.
Agenda ya kiongozi wako inakuhusu.Hakika unachohitaji ni Elimu,Elimu, Elimu. .
Anonymous November 3, 2015 at 12:43 PM
Yote uliyoandika hapo juu ni hadithi ya sungura na zabibu. Sungura aliposhindwa kuzifikia zabibu hizo pale mtini badala ya kusema ukweli huo akajidai kuwa alikuwa hazitaki kwa ajili ati zilikuwa ni mbichi.
Mwenzetu pole sana. hata hivyo kwetu tunoona kuwa zabibu hizo zimeiva tunapenda kuungana na wenzetu kusheherekea siku hii muhimu ya kuapishwa kwa rais wetu wa awamu ya tano. Mungu ibariki Tanzania na watu wake na pia wabariki viongozi wote kutoka nje ya nchi yetu wanaokuja kujumuika nasi katika hafla hii.
Post a Comment