ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 21, 2015

MTEMVU AFUNGUA KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA TEMEKE

 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, (hawapo pichani), ambapo aliwaeleza kuwa amefungua kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Jimbo la Temeke,ili haki ipatikane. Kushoto ni Katibu wa Jimbo la Temeke,  Kassim Kiame.

Walioshitakiwa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Temeke, Protidas Kagimbo Mbunge aliyeshinda, Abdallah Mtolela na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (PICHA NA KHAMIS MUSSA)

2 comments:

Anonymous said...

sawa ana haki ya kufugua kesi.mabango yake ya kujitangaza pekee yalizidi laki tano,kwenye kuta za maofisi,majumba,viwanja vya mpira,ofisi za serikali,vyoo,magari mabovu,barabara zooote temeke,mabaa,maguest na kwingineko.magari yake ya kampeni permantely yenye vipaza sauti vya nguvu yalikuwa nane,wafayakazi wa kampeni [wa kulipwa]zaidi ya 100.pesa za rushwa alikua anagawa kama ana kiwanda cha kufyatua.siku ya mpira wa simba na yanga alizipanga gari nne kwenye vichochoro maalumu kutugawia tiketi za kiingilio -tuliambiwa alinunua tiketi alfu kumi.watu wote wa temeke na tff yenyewe wanalijua hilo.jifunze mtemvu kukaa kimya. kila mwananchi wa temeke alijua ulivyojitahidi kutoa rushwa.tulikwisha kuchoka na ndio maana sehemu nyingine ulikua unashindwa kuhutubia kutokana na kuzomewa.mtemvu bado una hamu tena kurudi mwembe yanga?

Anonymous said...

Sasa huyu nae atajita ni kiongozi, atokomee kuleee!! Michosho tu, amekalia wizi, rushwa korrupt