ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 12, 2015

Awafagilia Watanzania na tabia zao

Na Freddy Macha
Ulikuwa na wenzio Tanzania kwa miezi sita...Mbeya vijijini. Ulikaa na wananchi. Vipi ulijisikaje katika eneo hili la Afrika? "...Lilikuwa jambo la kipekee. Ilitupa changamoto na utofauti mkubwa, ambao sin’tokwawia kulirudia tena.
Kama nilivyokueleza awali kila siku tuliyokuwa vijijini ilikuwa kama wadhifa fulani. Maana tulitaka kuwa sehemu mahsusi ya jumuiya...wenyeji walitukaribisha, walituhusisha katika mambo yao...tulikaa na familia zao, tunashukuru sana kwa hilo. Walifungua milango yao. Wakatukaribisha. Mara nyingi ilibidi kujifinya, na kujiuliza je kweli, Mungu wangu niko kweli Afrika? Na hisia hiyo ya kutoamini maastajabu haikunitoka kwa miezi yote sita niliyokuwa Tanzania! Ni uzoefu ulionibadili sana. Nadhani wanavijiji wengi walikuwa na wasiwasi kwamba sisi Wazungu tulikuwa wasafi au tungeshindwa kuishi maisha yao. Ilibidi wahimizwe kuwa hakuna noma yeyote..." 10-Evelina na wenzake wakiwa na timu ya wanafunzi vijijini- Picha ya Evelina Moceviciute 2015 
  Evelina na wenzake wakiwa na timu ya wanafunzi Watanzania vijijini - Picha ya Evelina Moceviciute 2015
 Wanafunzi wanavijiji Lukata na Evelina na wenzake 
Wanafunzi wanavijiji Lukata na Wageni waliowafundisha taaluma ya biashara. Picha ya Evelina Moceviciute

No comments: