
Rais Uhuru Kenyatta ameagiza walimu
nchini humo kulipwa mishahara yao ya mwezi Septemba, na kuitaka Tume
ya Huduma za Walimu (TSC) pamoja na vyama vya walimu kujadiliana juu
ya ongezeko la mshahara.
Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano
uliofanyika Ikulu ukihusisha makamishna wa TSC pamoja na maafisa wa
Chama cha Taifa cha Walimu Kenya (Knut) na kuafikiana kumaliza
mgogoro wa muda mrefu wa malipo ya walimu.
Rais Uhuru ameziagiza pande zote
hizo kufanya mazungumzo ndani ya mwezi mmoja, ili kufikiwa
makubaliano yatakayoweza kuafikiwa na kutekelezwa na pande zote.
1 comment:
Inapofikia kuhusu maswala ya waalimu lazima kuna tatizo la kupunjwa au kutokulipwa mishahara! Ni jambo lililoko kila kona ya nchi za Afrika. Mbona watumishi wengine wao wanalipwa mishahara tena mizuri!! Hawa ndio wanaowafundisha wataalamu wengi na hata wanaokuja kuingia serikalini hadi mawaziri iweje wanafanyiwa vitendo vibovu!
Ukienda Uganda, Tanzania Msumbiji utakuta yote hayohayo!!
Post a Comment