Advertisements

Friday, November 20, 2015

RAIS MAGUFULI AAGIZA FEDHA ZA HAFLA YA WABUNGE ZIPELEKWE MUHIMBILI KUNUNULIA VITANDA VYA WAGONJWA


Baada ya kulihutubia na kulizindua bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt JOHN POMBE MAGUFULI amehudhuria hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya wabunge katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma na kuagiza fedha zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla hiyo zipelekwe Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda vya wagonjwa.

Mheshimiwa Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa wadau mbalimbali wamechanga kiasi cha shilingi milioni 225 kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge katika siku ya uzinduzi wa Bunge.

Dkt Magufuli amesema alipata taarifa za kuwepo kwa michango hiyo ya fedha na kutoa maelekezo kuwa zitumike kwa kiasi kidogo kwa ajili ya hafla hiyo na sehemu kubwa zipelekwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili zikatumike kununulia vitanda na hivyo kupunguza tatizo la wagongwa wanaolala chini kutokana na uhaba wa vitanda unaikabili hospitali hiyo.

“Nilipoambiwa kwamba zimechangwa shilingi milioni 225 zimekusanywa kwa ajili ya sherehe, nikasema fedha hizo zipelekwe katika hospitali ya Taifa Muhimbili zikasaidie kununua vitanda” alisema Dkt Magufuli na kusisitiza kuwa “kwa kufanya hivyo tutakua tumejinyima sisi wenyewe lakini tutakua tumewanufaisha wenzetu ambao wanamatatizo makubwa yanayoweza kutatuliwa kwa fedha hizo”.

Awali akitoa taarifa ya michango hiyo Ofisa wa Spika wa Bunge Bwana SAID YAKUBU amesema jumla michango iliyopatikana na shilingi milioni 225 na kwamba fedha zilizotumika katika hafla hiyo ni shilingi milioni 24 tu baada ya kuzingatia maagiza ya Rais Magufuli.

Katika Hafla hiyo Rais Magufuli amekabidhi vyeti vya kutambua mchango wa wadau waliochangia fedha wakiwemo Benki za NMB, CRDB na Benki ya Afrika pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF na PPF.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU
November 20, 2015

6 comments:

Unknown said...

Kama viongozi wa kiafrika wangekuwa na machungu na hali za maisha ya wananchi wao na nchi zao kama alivyo huyu jamaa basi Africa ingekuwa ipo mbali sana. Africa ina rasimali za kutosha lakini zinaishia katika kuwanufaisha viongozi na kuwaacha wananchi walio wengi katika hali ya umasikini uliokisiri. Magufuli ni tumaini jipya si kwa Tanzania tu bali Afrika nzima ni kiongozi mwenye moyo wa dhati kuhakikisha anainua hali za maisha ya wananchi wanyonge walio wengi. Hongera sana Magufuli.
Sasa kazi tu.

Anonymous said...

Dunia bwana .ulimwengu shujaa.mwanaume,unakuwa unamuheshimu,lakini anakuona.fala,ajui.hapa akili,imekonjoa,anakudharau,anaona wewe ndiyo umefika.ila kuwa makini kumfanya mwenzako fala,ujui leo na kesho utakuja kusema ningejuwa.chezea dunia.unapewa chasi unazid kumuona mwenzako fala pamoja na yote uliofanya.shauri yako hee mama siwezikuwa fala mwisho una choka.

Anonymous said...

Kweli watu wametofautiana yule mwingine angejirusha hadi majogoo. Halafu kesho yake angepanda ndege kwenda Marekani

Anonymous said...

Unajaribu kuandika kitu gani wewe mbumbumbu? Nadhani wewe hukuhudhuria hata madarasa ya elimu ya watu wazima, kama ulizaliwa kabla ya Operation Vijiji vya Ujamaa!

Anonymous said...

Mdau mbona hueleweki!

Anonymous said...

HUU NI MWANZO TUU WA KAZI NZITO NA YA HATARI INAYOKUJA KUTOKA MEZA YA MHESHIMIWA MAGUFULI.WATANZANIA TUMUOMBEE KWA MWENYEZI MUNGU NA TUMUUNGE MKONO.AMEINGIA IKULU MHESHIMIWA AMEYAKUTA MADUDU,TENA MAKUBWA YA KUTISHA KATIKA UHUJUMU NA POROMOSHA UCHUMI TUMELIWA SANA.SIFA KUBWA YA MHESHIMIWA MAGUFULI NI HII SI MNAFIKI,LA UKWELI HALICHELEWESHI NA NDIYO HAYA ALIYOANZA KUTUWEKEA HADHARANI.WEZI WALIOKUWEMO SERIKALI YA AWAMU YA NNE MIDOMO IMEANZA KUPAUKA.LA MAHAKAMANI WALA HALIPO MBALI NAWAAMBIENI TUHESABU SIKU TUU.KAMATA KAMATA ISIMUONEE MTU HAYA,WAKAMATWE TUU.