ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 27, 2015

RAIS MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU WA TRA

Raisi wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 27 Nov. 2015, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema leo asubuhi Bandarini jijini Dar es salaam.

Hatua hiyo imekuja baada kubaini kupitishwa kwa makontena zaidi ya 300 na kusababishia hasara Serikali ya zaidi ya shilingi bilioni 80.

Rais Magufuli pia amemteua  Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo mpaka hapo uchuguzi utakapo kamilika.

Taarifa hiyo iliyosomwa na Katibu Mkuu Kingozi, Balozi Ombeni Sefue Ikulu jijini Dar es salaam, imewataka maofisa wote wa TRA kutosafiri nje ya nchi mpaka pale uchunguzi dhidi yao utakapo kamilika.

2 comments:

Anonymous said...

Duh! Ufagio hautazami sura!

Unknown said...

Mueshimiwa raisi Maghufuli hata hajaanza bado hizo ni salam tu. Aliesoma kasoma, Magufuli smart usifikirie mtu mwenye elimu ya kiwango cha PHD tena katika taaluma yenye kuhitaji uwezo mkubwa wa akili kama Mathematics na Chemistry ataendesha mambo yake kiholela kama watu wengi walivyokuwa wakijisemea hasa kuna wale watanzania wanaojiita maprofesa wachambuzi ambao kwa kweli wamefeli kabisa katika chambuzi zao zinazohusu uwezo binafsi wa utendaji wa kazi wa Magufuli. Inaonesha dhahiri Mr Magufuli anataaluma tosha kabisa kiasi kwamba hao wanaojiita wasomi na maprofesa wachambuzi inabidi kukaa chini na kujifunza kutoka kwa muheshimiwa Magufuli kabla ya kutoa chambuzi zao juu yake ambazo mara nyingi zinakuwa hazina mshiko wowote. Walisema Magufuli hawezi kuunda mahakama za mafisadi zaidi ilikuwa janja yake ya kutafuta kura. Leo tumeona wenyewe kwa kutumia wataalam wa sheria na kushirikiana na bunge Mr Magufuli tayari yupo mbioni kuhakikisha mahakama hiyo inaundwa haraka. Ukiangalia vizuri kasi aliokuja nayo Magufuli utagundua sio mtanzania wa kawaida na kwa kweli kama atapata ushikiriano mzuri atafanya mazuri zaidi ya yale aliyoyahidi kwenye kampeni.