ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 14, 2015

TAKWIMU ZAJIELEZA ZENYEWE MAGUFULI KUSHINDA KWA KISHINDO , RAIS MWENYE HOFU YA MUNGU

Rais Dr John Magufuli

- Mgombea wa CCM ndugu John Pombe Magufuli ametembea Kilometa 44, 467 katika majimbo 241 ndani ya mikoa 30, ambapo ametumia gari na boti wakati Mgombea wa Ukawa ametembea Kilometa zisizodizi 3,000 kwa gari, ametembelea majimbo 137 yaliyo kwenye mikoa 25.

- Jumla ya mikutano rasmi ya hadhara ni 252 na mikutano midogo ya kusalimia njiani zaidi ya 896 ndio ambayo ameshahutubia Dr John Pombe Magufuli, ukilinganisha na Mgombea wa UKAWA ambae amehutubia Mikutano Mikubwa 102 tu tangu kuanza kwa kampeni na idadi ya mikutano isiyo rasmi ambayo haipo kwenye ratiba ya kusalimia wananchi ni michache sana kwa sababu mgombea huyu anatumia Chopa, hivyo kukosa fursa ya kusalimia wananchi vijijini.

- Ndugu John Pombe Magufuli ameshahutubia kwa masaa takriban 306 sawa na wastani wa 45min - 1hour kwa kila mkutano mkubwa wa hadhara wakati mgombea wa UKAWA amehutubia kwa masaa 26 sawa na dakika 8.93 - 12 kwa kila mkutano.


- Dr Magufuli amekadiriwa kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 12 ana kwa ana na takriban Milioni 36 kwa njia za Mawasiliano ya Radio, Magazeti, TV na mitandao ya kijamii..wakati mgombea wa UKAWA amewafikia wananchi wasiozidi milioni 5 ana kwa ana katika Mikutano ya hadhara michache aliyoifanya na amewafikia wananchi wasiozidi milioni 11 ktk njia za TV, Magazeti, Radio na mitandao ya kijamii ambapo mara zote mikutano ya UKAWA hairushwi live kwenye TV, wala radio.

- CCM ina wanachama zaidi ya milioni 8 nchi nzima, UKAWA wana wanachama milioni 4 nchi mzima…ikiwa wanachama wa CCM wanaoamini ktk LOWASSA watampigia kura, CCM inakadiriwa kupoteza kura laki nane (ingawa historia inatufundisha kuwa wanaccm huwa wagumu sana kumchagua Kada mwenzao pindi akihama Chama, kumbuka Mrema – 1995)…na ikiwa wanachama wanaoamini katika Lipumba, Makaidi, Mtikila, Dr Slaa na Zitto wataamua kuchagua Uadilifu wa Magufuli, CCM inakadiriwa kupata kura zaidi ya Milioni moja na nusu kutoka kwa wanachama wa Upinzani.

- CHAMA…mtandao wa CCM unaofika ngazi ya nyumba kumi za kila mtaa wa Tanzania na mfumo imara wenye mahusiano mazuri na “system†unamuhakikishia Magufuli ushindi ambapo Mfumo dhaifu uliotokana na Ombwe la uongozi ktk Upinzani unaoamini matusi, vurugu, kashfa na kuimarisha Uadui dhidi ya “system†unaharibu na kufuta kabisa hata yale matumaini kidogo ya kupata hata theluthi ya kura kwa Edward Ngoyai Lowassa.

- Voters Behavior, kwa kawaida CCM inapigiwa kura na wanawake zaidi kuliko jinsia nyingine na makundi rika mengine. Wanawake waliojiandikisha ni Milioni 11,950,200 sawa na asilimia 53 ya watu wote waliojiandikisha, idadi hiyo ni milioni mbili zaidi ya wanaume ambao ni Milioni kumi tu, ambapo kwa kundi rika walio chini ya miaka 30 (yaani Vijana) ni milioni 4 tu.

HISTORIA ya maisha yake tangu alipozaliwa hadi sasa, John Pombe Magufuli ameishi katika matakwa ya dini ya Kikrosto.
Mbali na kuwa mkristo, mkatoliki, anamheshimu kila mtu. Mwenye imani kama yake, imani tofauti na hata wale wasio na dini, wote anawapa haki sawa. Amemtanguliza Mungu katika kila jambo. Safari yake ya kuomba urais, aliianza kwa kumtanguliza Mungu na kweli akajibu maombi yake. Kumbuka katika safari hiyo kulikuwa na watu 42 waliokuwa wakiwania nafasi hiyo, kila mmoja aliomba kwa imani yake lakini Mungu akamuongoza Mugufuli, akapitishwa.

Mchakato wake wa kutangaza nia ulikuwa wa kimyakimya. Hakutoa ruswa kwa mtu yeyote ili aipate nafasi hiyo japo baadhi ya wenzake walidaiwa kutoa ili waweze kupitishwa na vikao vya chama.
Tangu akiwa shule ya msingi, Magufuli aliishi maisha ya kumpendeza Mungu licha ya kukutana na changamoto mbalimbali zilizosababishwa na ukata.
Alitembea umbali wa kilometa 5 kila siku kutoka kijiji cha Rubambangwe hadi Shule ya Msingi Chato. Hakuwahi kuchelewa. Alikuwa ni mtu wa kujituma, hakupenda kukwazana na mtu. Zaidi alizingatia masomo yake ya kemia na baadaye kuwa mtaalamu aliyebobea katika masomo hayo.
Mwalimu wake, marehemu Cornely Pastory aliwahi kueleza dhahiri kwamba, Magufuli ni miongoni mwa wanafunzi wake waliokuwa wapole, wanyenyekevu ambao hawakuwa na historia mbaya shuleni. Aliiishi kwa matakwa ya Mungu.
Historia yake kimaisha imeendelea kuwa hivyo. Hakuwa mtu wa kujikweza hata alipokuwa waziri. Mke wake aliendelea kuwa mwalimu wa shule msingi. Watoto wake amewalea katika maadili ya dini, amekuwa mzalendo na ndiyo maana hakuna mwanaye hata mmoja aliyekwenda kusoma nje ya nchi kuanzia hatua ya awali hadi chuo kikuu.
Huyo ndiye Magufuli ambaye kwa macho ya kawaida kabisa unaona anatosha kuwa rais. Mahali popote amekuwa akimtanguliza Muingu katika majukumu yake. Baada ya Mungu, anatekeleza sheria ili asimuonee mtu.
Amekuwa akisimamia sheria katika barabara. Tumeshuhudia akivunja nyumba ambazo zimeifuata barabara bila kujali ni ya nani. Anasimamia sheria, hatishwi na tajiri. Anaangalia sheria inasema nini, kama amepindisha basi anapambana naye.
Hofu ya Mungu ndiyo inayomuongoza kusimamia sheria. Anachukia ufisadi na rushwa. Akiwa Wizara ya Ujenzi, amewatimua wafanyakazi wengi wala rushwa. Anatamani kila mmoja ale kulingana na haki yake.
Alipokuwa akihutubia kwenye Uwanja wa Jangwani jijini Dar katika uzinduzi wa kampeni zake, alianza kwa kumtanguliza Mungu mbele. Aliwashukuru Watanzania wote waliojitokeza uwanjani hapo kwa kumuamini, hakumbagua mtu kwa dini, kabila lakini zaidi aliwasalimu katika jina la Mungu.
“Ningependa kushughulika na uchumi wetu, ukue. Kila mmoja wetu awe na uchumi mzuri hususan kwa wanyonge, natamani zaidi niwasaidie hao,” alisema Magufuli kwenye mkutano huo.
Aidha, kwenye hotuba hiyo, Magufuli alitumia muda mrefu zaidi kuwazungumzia Watanzania wa hali ya chini. Hivyo ndivyo alivyokuwa akizungumza katika mikutano yake mingi. Amekuwa akisema matatizo ya Watanzania anayajua.
Aliposema anayajua alimaanisha kwani alieleza wazi kwamba ameyaishi. Amechunga ng’ombe kama wachungaji wengi wa kawaida. Hivyo atafanya kila linalowezekana kuhakikisha anamaliza tatizo la umasikini.
Akaendelea mbele zaidi kwa kuwaahidi Watanzania kwamba anatambua nchi ina watu wenye imani tofauti hivyo wote watakuwa na haki sawa, matatizo yote atayatatua pasipo kujalia itikadi za kivyama, ukabila wala udini.
Magufuli alisisitiza amani. Akazungumzia kudumisha umoja miongoni mwa Watanzania. Alipohamia mikoani, Magufuli alionekana kumtanguliza Mungu katika kila anachokifanya. Aliomba Watanzania wampe kazi ya urais ili awatumikie.
Alieleza sera zake huku akihofia kumdanganya mtu. Alikataa uongo kwani ni dhambi. Alitamka ahadi ambazo anaamini zinatekelezeka.
Kile ambacho aliona hakitekelezeki kutekeleza, alisema dhahiri huku akionesha juhudi za kupatia ufumbuzi.
“Ndugu zangu mimi nasema ukweli. Nasema ukweli kutoka moyoni, nikiahidi kitu lazima nitekeleze. Kwangu mimi ni kazi tu. Siwezi nikasema nitamaliza nyumba zote za tembe nchi nzima kwa wakati mmoja. Huo utakuwa ni uongo. Wanaosema hivyo ni waongo. Tutazipunguza kwa awamu na nina imani ipo siku zitakwisha kabisa,” alisema Magufuli katika moja ya mikutano yake ya kampeni.
Kwenye kipindi cha kampeni, wagombea mbalimbali wamekuwa wakitoa ahadi ambazo ukizitathimini kwa jicho la tatu hazitekelezeki. Kwa Magufuli hilo halipo, yeye amekuwa akiahidi ahadi ambazo anaamini zinatekelezeka.
Hakutaka kuonekana muongo. Hakutaka kutenda dhambi hiyo na ndiyo maana kila alipopita amesisitiza Watanzania wamuombee ili aweze kuifanya kazi ya urais katika matakwa ya Mungu.
“Ndugu zangu nimeomba kazo hii ya urais nikiamini naiweza. Nikiwatazama hapa mlivyokusanyika, mnadhihilisha kwamba mnanipenda. Ndugu zangu mniombee...”-Magufuli.
Ameyasema hayo huku machoni akionesha anamaanisha. Hiyo imemuongezea imani kubwa Magufuli kwa Watanzania. Akizungumzia umasikini anaonekana anaguswa na tatizo hilo, ana kiu ya kutaka kulitatua.
Mungu ni upendo, Magufuli anahiza amani, umoja kwa Watanzania wote kwa sababu ana hofu ya Mungu, huyo ndiye rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

7 comments:

Anonymous said...

Takeimu za aina yake##

Anonymous said...

Wako wapi hawa watu we EL waliokuwa wanapiga makelele humu jamvini? Ohh tumechoka na ccm, ohh hata lingewekwa jiwe, ccm lazima ishindwe tu.. Vibaya hivyo jamani mkishindwa mnakimbia? au wengi wao mlikuwa wabeba mabox sio wapiga kura? Hamuachi?

Anonymous said...

NUMBERS DON'T LIE.

Anonymous said...

Sasa mbona tume ilichakachua matokeo halisi? Kwa nini Mama Kijo alipata ajali ya sintomfahamu? Kama yeye ni mchamungu aruhusu watu wenye takwimu tofauti na zenye uthibitisho ziwekwe hadharani.
Mwisho, Wewe muandishi unajua kuwa JPM ndo Rais wa kwanza wa CCM kushinda kwa kura chache % sana kuliko marais wote walotangulia.
Maelezo yako hayashabihiani na hali halisi ya matokeo ya kura.

Anonymous said...

ACHA UCHOKOZI WEWE KAKA.TUMUACHE MHE.RAIS MAGUFULI AFANYE KAZI.KAMA WEWE NI MPAMBE WAKE NA KWA KUA INAELEKEA NI MLAFI WA VYA BURE, UMEVIKUTA JIKONI IKULU. KUVIMBIWA PEKE YAKE KUTAKUSABABISHIA GONJWA LA VIDONDA VYA TUMBO.HIZO TAKWIMU UNAONAJE UKAZISHONA KWENYE LILE SHATI LAKO LA KIJANI ULILOPEWA BURE NA PESA JUU ILI UWE UKITEMBEA NAZO.MIMI LEO HII NIKIANZA KUMSIFIA LOWASSA,MFULULIZO,ITACHUKUA MIAKA MITANO.HEBU KWANZA,TUACHE,TUTULIE,TUJENGE NCHI.UMENIELEWA KAKA?

Anonymous said...

Anonymous wa November 14, 2015 at 1:53 PM - acha ubishi. Wananchi waliamua na rais wamempata. Kura zilihesabiwa na maajenti wenu walisaini makaratasi kuthibitisha kuwa kura hizo zilikuwa sahihi. Hizo kura zenu mnazosema ziko tofauti na za Tume mbona hamzitoi watu wakaziangalia badala yake mnabaki kulalamika tu. Au ndiyo mnaona aibu kwa vile kura zenu hizo ni zile za ubabaishaji zilizogushiwa na mamuluki wenu mnawaita wataalamu wa IT ambao wameshikwa kwa kutaka kuhujumu uchaguzi na sasa wanasota jela wakisubiri mashitaka yao kusilkilizwa?

Kuhusu swala la ajali ya Mama Kijo unaliunganisha vipi na uchaguzi huu? Kuna ajali nyingi tu zimetokea nchini wakati wa kipindi cha uchaguzi na watu wameumia na wengine wamepoteza maisha yao, je mbona hizi hujazitaja na umeona ya Mama Kijo peke yake tu ndiyo? Pamoja na mawazo uliyo nayo kuhusu swala hili ningekushauri kuacha mikingamo na ushabiki usio na maana.

Juu ya JPM kupata asili mia ndogo ya kura inaonyesha jinsi ushindani ulivyokuwa mgumu na hii inaonyesha kukua kwa upinzani na pia ishara nzuri ya kushamili kwa demokrasia. Hii ni ishara nzuri.

Anonymous said...

Hakuna cha tume kuchakachuliwa wala nini magufuli kashinda kihalali kabisa isipokuwa chadema na viongozi wao ni watu waongo na hakika mtu yeyote mwaadilifu ni vigumu kuwaamini wanachokisema. Na cha ubaya zaidi baada ya kuugemeza nguvu zao vujijini kwa watanzania walio wengi wao wanatumia rasilimali zao katika kuwaandaa vijana katika mitandao ya kijamii kusambaza taarifa za uongo. Utawaamini vipi watu waliosema serikali ya CCM inawakamata vibaka wadogo na kuwafunga na kuwaacha vibaka wakubwa kama akina lowasa wakiendelea kutesa.