ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 30, 2015

UN WAKISHIRIKIANA NA UBALOZI WA PALESTINA WAFANYA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MSHIKAMANO NA WATU WA PALESTINA




Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati), Kaimu Balozi wa Palestine Derar Ghannam (kulia) pamoja na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali wakikata utepe kwa ajili ya maonesho ya picha za matukio mbalimbali yanayoendelea nchini Palestina hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar. 
Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam (wa kwanza kulia) akimuonyesha picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati) za matukio ya mauaji ya watu nchini Palestina yanayofanywa na Waisraeli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
Baadhi ya picha zinazoonesha matukio ya mauaji pamoja na majeruhi yanayoendelea kutokea nchini Palestina kutokana na vita inayoendelea nchini mashariki ya Kati kati ya Palestina na Israeli. 
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi Stella Vuzo (kulia) akitazama picha za wananchi wa Palestina waliouliwa na kutokana na mapigano ya Palestina na Israel yanayosababisha vifo vya watu wengi wasiokuwa na hatia. 
Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kusikiliza kwa makini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina. Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima akisoma hotuba yake mbele ya Mabalozi, wanafunzi wa chuo cha Diplomasia pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye maadhimisho ya ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar. 
Naibu Mkurugenzi wa Mipango Utawala na Fedha wa Chuo cha Diplomasia, Dk.Bernard Achiula akizungumza jambo wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika chuoni hapo. 
Prof Josephat Kanywanyi ,Chairperson Tanzania- Palestine Solidarity committee akitolea ufafanuzi kuhusu mahusiano ya Tanzania na Palestina wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina. 
Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina. 
Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakiendelea kusikiliza kwa makini kinachozungumzwa kutoka meza kuu. 
Mshauri Mwandamizi wa Utawala kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa mataifa (UNDP), Steve Lee aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza uhusiano wa Palestina na Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar. 
Baadhi ya Mabalozi waliofika kwenye maadhimisho hayo wakiendelea kufuatilia yanayojiri. 
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya Pamoja na Viongozi mbalimbali pamoja mabalozi. 
Viongozi wakiwa kwenye picha na wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia. 


Na Mwandishi wetu

UN Tanzania ikishirikiana na Ubalozi wa Palestina nchini waadhimisha Siku ya Kimataifa na Mshikamano na watu wa Palestina na Tanzania katika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma na kukutana na mabalozi wa wa nchi mbalimbali akiwepo Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima, Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali ambapo ikiwa kuendeleza ushirikiano pamoja na mfululizo wa maonesho ya picha mbalimbali za matukio yanayoendelea huko nchini Palestina.

Mabalozi hao ambao walikutana katika jijini Dar es salaam kwaajili ya kuadhimisha siku hiyo ya kumbukumbu za picha za mapigano ya Palestina kwa ajiri ya kudumisha upendo na mshikamano pia mabalozi hao wameuomba umoja wa mataifa kuweza kuchukua hatua za ziada zitakazo pelekea nchi hiyo kuwa huru na kuweza kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Mshauri Mwandamizi wa Utawala kutoka UNDP, Steve Lee akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kuwa uhusiano wa Palestina na Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina alisisitiza kuwa na na umoja baina ya nchi zote mbili hususani Palestina kuweza kupata uhuru na kutambulika kuwa ni nchi nyenye mipaka yake binafsi ili kuepusha mapigano hayo yasiweze kutokea na kila mtu aweze kuishi na amani akiwa ndani ya nchi yake na kuweza kufanya maendeleo ya nchi. Na aliweza kuziomba nchi mbalimbali kulitambua taifa la Palestina kama nchi kamili tofauti na inavyotambulika kwa sasa.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa siku ya maonesho ya picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima amesema wamefanya hivyo kwani ni hari ya kuwatakia heri Wapalestine wote kwani watu wote waparestine walipoteza uhuru na kwa sasa wanautafuta uhuru kwani nchi wanayo lakin hawako huru kwahiyo ni lazima tuwaunge mkono kwa kuweza kuadhimisha siku hii sehemu mbalimbali tunayoishi.

Kwa upande wa Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Bi Stella Vuzo amesema wameamua kuwa na maadhimisho kwani ndani ya miaka 50 Palestina wamekuwa hawajatambulika kama taifa lenye mipaka yake ambapo kumekuwa na migogoro ya mda mrefu ambao unawahusu wa Palestine na wayahudi ambao upo tangu mwaka 1947,wakati katika maadhimio walio fikiana ni kuwa na mataifa mawili ndani ya eneo moja ambap mpaka sasa Israel pekee ndo iliyo pata kuwa hali ya taifa lenye mipaka yake wakati . Kila siku Israel huwa wanaleta vita ndani ya Palestine, sasa maadhimisho haya ni kwa ajili ya kuwaunga mkono kwa vitendo vinavyo endelea huko si vizuri. Pia aliwaomba viongozi wa pande zote mbili kuweza kuketi na kuweza kuweka maadhimio mapya kwaajili ya kuepusha mapigano yanayokuwa yakitokea kila siku baina ya nchi hizo mbili. Pia katika siku hiyo waliweza kuzindua picha za matukio ya vifo pamoja na watu walioumia kutokana na vita Palestina na Israel zilizo kuwa zimeandaliwa kwa Tanzania kwa ajili ya kuonyesha dunia matukio yanayoendelea katika nchi za Mashariki ya mbali hii yote ni kwa kuwa Palestina ina ushirikiano na Tanzania na kuwaombea katika kuelekea hali ya utulivu.

No comments: