ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 20, 2015

ALICHOONGEA IVAN KWENYE MAHOJIANO NI HIKI

Nilitaka kukujuza tu alichoongea Ivan alipofanya mahojiano na mtangazaji wa Luninga nchini Uganda siku aliyotua Kampala kwa ajili ya White Party iliyoandaliwa na Zari. Watu wengi wametafsiri kivyao mahojiano hayo ikabidi Vijimambo imtafute mkalimani kutoka Uganda atutafsilie ili na sisi tuweze kuwajuza ni nini hasa alichoongea Ivan kwenye mahojiano hayo.

Swali la kwanza aliulizwa  kuhusu kundi lao la Rich Gang ambalo linaundwa na yeye Ivan Ssemwanga, King Lawrence na Cheune na kueleza kwamba sharti la kujiunga na rich gang lao ni lazima uwe na bilioni 10 za Kiganda na ukipungukiwa kwa aina yeyote ile basi unakua umejiondoa kwenye kundi lao.

Mtangazaji pia alimuuliza swali la kizushi kama bado anamahusiano na Zari na kwanini anapotajwa Zari linahusishwa jina lake. Ivan alijibu kwamba Zari walishaachana miaka miwili iliyopita na sasa anamahusiano na Diamond kinacho mhusisha na Zari ni watoto wao tu si kitu kingine.

Na kuhusu Zari kutegemea pesa kutoka kwake Ivan hilo amekataa na kusema sio kweli Zari ana pesa yake, Fedha anayotoa ni ya Watoto tu wala si ya Zari. Kama unaelewa Kiganda isikilize video hapo chini,

Zari and Diamond in kampala
Picha ikimuonyesha Diamond na Zari wakiwa kwenye show Uganda siku ya Ijumaa Desemba 18, 2015.
Zari and Diamond in kampala
Diamond na Zari wakikata mitaa na Zari Kampala, Uganda.
 Picha zaote kwa hisani ya Bigeye.

No comments: