Ukikaa karibu na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kumekuwa na ripoti mpya kila wakati na kadri zinavyonifikia na mimi nahakikisha hupitwi hata kidogo.
Kama unakumbuka December 03 2015, Rais Magufuli alikutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania na moja ya vitu alivyokosoa na kuonekana kukasirishwa navyo sana ilikuwa ishu ya kubinafsishwa kwa ufukwe wa Coco Beach, Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mussa Natty
Ripoti imenifikia kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya na Kinondoni Dar es Salaam na baadae kuhamishiwa Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara, Mussa Nattyamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali.
Kwenye taarifa hiyo kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaaimeonesha sehemu ya tuhuma zinazomkabili Mkurugenzi huyo ni pamoja na usimamizi mbaya uliosababisha barabara za Manispaa ya Kinondoni kuwa chini ya kiwango, ukosefu wa uadilifu na kubinafsisha ufukwe wa Coco Beach pamoja na usimamizi mbovu wa watumishi wa idara za ardhi.
Hii hapa ripoti yenyewe kuhusu taarifa hiyo.
Credit:MillardAyo.com


2 comments:
NI DHAHIRI SAGINI WA TAMISEMI ALIMBEBA NATTY AKAMFANYIA UHAMISHO WA CHAP-CHAP KWENDA BABATI.HILI LILIKUWA NI KOSA KUBWA SANA LA KIUTENDAJI.MHESHIMIWA MAGUFULI AKAGUNDUA NA KUTOA AGIZO HILI JIPYA.NATTY NI MWIZI,MLARUSHWA TENA ZA WAZI WAZI WEWE LEO HII UNAMHAMISHA,MAANA YAKE NINI?MAANA YAKE NI MSHIRIKA WA KARIBU WA SAGINISAGINI YEYE AFUKUZWE KAZI,ALIKULA NJAMA MBAYA.
Hawa watu wasiwe wanafutwa kazi tu bali pia kupigwa faini na kufirisiwa mali zao na kusweka rumande kwa miaka mingi tu ili wakafie huko.
Post a Comment