Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la #TegetaEscrow. Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu. Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri? Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena?
Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu. Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa
1) Azuie kuanzia sasa malipo ya 'capacity charges' kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO
2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania
3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani? Tuache siasa za porojo porojo

4 comments:
Huyu Bwana akili zake nyingi kuliko Mbowe, Lisu na Lowassa. Ndio maana hawakuweza kukaa naye. Ni mtu objective and balanced. Watu wa porojo porojo tunajua wako wapi.
Zitto naye arudishe pesa zote ambazo CCM wamekuwa waki-deposit kwenye account yake iliyoko Ujerumani.Huyu jamaa ndiyo maana Chadema walimshtukia mapema na kumpiga chini mara moja.Haaminiki hata kidogo.
KAMA UTASHANGAA LEO HII UKIAMBIWA ZITTO NI CCM,WATU WENGI TUTAKUSHANGAA NA KUKUONEA HURUMA VIVYO HIVYO KWA SLAA NA LIPUMBA,TURUDIE MARA NGAPI? MILLION?ZITTO NI MSALITI DARAJA 'A' NA ANGALIENI KWA MIAKA HII MITANO MTAMSHUHUDIA ATAKAVYOKUWA ANAIBEBA CCM
Zitto nenda ccm naona chama chako na jimbo lako umevisahau kabisa,umekuwa cheer leader mzuri wa ccm.
Post a Comment