Saturday, December 5, 2015

Daraja la Jangwani Dar laanza kusafishwa


Daraja la Jangwani, Dar kama linavyoonekana na maji ya Mto Msimbazi yakipita kwa shida kutokana na kuzingirwa na takataka.Tingatinga lililokuwa likitumika kusafisha na kupanua kingo za Mto Msimbazi darajani hapo.Mwonekana wa daraja hilo.Taswila ya Mto Jangwani unaotokea maeneo ya Msimbazi ukiwa umepanuliwa.Tingatinga likiwa kazini darajani hapo.

Katika kuelekea maadhimisho ya Sikukuu ya Uhuru, Desemba 9 mwaka huu, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam imeanza kutekeleza kwa vitendo kauli ya Rais John Pombe Magufuli kwa kusafisha eneo la Dararaja la Jangwani lililopo Mto Msimbazi uliokuwa umejaa uchafu na kuhatarisha kuziba njia ya maji chini yake.

Kamera yetu imefanikiwa kupata baadhi ya picha zikionesha taswila nzima ya eneo hilo kabla na wakati linafanyiwa usafi kwa kutumia tingatinga.

NA DENIS MTIMA/GPL

No comments: