Tuesday, December 8, 2015

DICOTA WAMKABIDHI BALOZI WILSON MASILINGI RIPOTI MBALI MBALI IKIWEMO RIPOTI YA FEDHA YA MKUTANO WA DICOTA NA TAARIFA ZA SHUGHULI ZAO.

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini  ya DICOTA Lunda Asmani alifikika mchana huu Disemba 8, 2015 ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington DC kumkabidhi Mhe. Wilson Masilingi  taarifa ya maandalizi ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2016 utakaofanyika  mwezi Aprili 28- Mei 1, 2016 jijini Dallas. 

Katika mazungumzo hayo, DICOTA walitoa maelezo mbali mbali ikiwemo kukabidhi ripoti ya mapato na matumizi ya fedha ya mkutano wa DICOTA wa 2014 na bajeti ya mapato na matumizi ya mkutano wa 2016. Hapo awali DICOTA walishamkabidhi Balozi Masilingi muhtasari wa mkutano wa 2014 pamoja na matukio mbali mbali ambayo DICOTA imekuwa ikishiriki kwa pamoja na wana diaspora na taasisi mbali mbali za ndani na nje ya nchi zenye lengo la kuendeleza wanadiaspora.

Pia bwn. Lunda Asmani alielezea jinsi DICOTA inavyojihusisha kwa karibu na viongozi wa Jumuiya za Watanzania wa majimbo nchini Marekani huku wakijaribu kuboresha mahusiano na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ambao hapo nyuma ulilegalega. Katika maandalizi ya mkutano wa 2016, DICOTA inashirikiana na Uongozi wa Jumuiya za Dallas, Kansas City, Wichita, Houston na Oklahoma.

Mhe. Balozi Masilingi alianza kwa kuwashukuru uongozi wa DICOTA kwa kupata wasaa wa kufika Ubalozini na kutoa taarifa ya shughuli zao pamoja na jitihada zao za kutekeleza maelekezo na miongozo mbali mbali iliyotolewa kwao na Balozi.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliwaasa viongozi wa DICOTA kuendelea kuwasiliana na wadhamini wa mkutano huo hasa walioweza kufika na kunadi bidhaa zao ili waweze kujua maendeleo ya bidhaa walizonadi kwenye mikutano yao.  Kwa kufanya hivyo kunaleta mahusiano mazuri na wadhamini ili wasiishie hapo wazidi kuwatangza na wao kujitangaza kupitia mikutano ya DICOTA.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliendelea kwa kusisitizia viongozi hao kuendeleza mahusiano na Jumuiya za Watanzania nchini Marekani hususani viongozi wa Jumuiya hizo na kutafuta uwezekano wa kukutana nao mara kwa mara.

Mwisho uongozi wa DICOTA waliuomba Ubalozi wasisite kuwaita mara wanapohitaji msaada wao kwani wanapotoa msaada kwa Ubalozi hujisikia kufarijika kwani ni furaha ni kutumia utaalamu na uzowefu wao katika kusaidia kusukuma kurudumu la maendeleo kwa kwa pamoja tunaweza.




1 comment:

Anonymous said...

Tunaomba ubalozi usaidie kufuailia kero ya passport renewal. Maofisa (Ofisa) husika hapo ubalozini wanasumbua (ana) sana.