Maalim Seif Sharif Hamad na Rais John Pombe Magufuli wakielekea kuongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mazungumuzo kuhusiana na hali ya kisiasa Zanzibar, mazungumuzo yaliyochukua saa mbili Ikulu jijini Dar.
Rais John Pombe Magufuli akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mazungumuzo kuhusiana na hali ya kisiasa Zanzibar, mazungumuzo yaliyochukua saa mbili Ikulu jijini Dar.
Maalim Seif Sharif Hanad akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mazungumuzo kuhusiana na hali ya kisiasa Zanzibar, mazungumuzo yaliyochukua saa mbili Ikulu jijini Dar.
Na K-Vis Media
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani, leo Desemba 21, 2015 pale Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam, , amekutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia alikuwa Mgombea kiti cha Rais wa visiwa hivyo, Maalim Seif Sharif Hamad na kufanya nae mazungumzo.
Kwa mujibu wa maafisa wa Chama Cha Upoinzani CUF, ambacho Maalim Seif ndiye Katibu Mkuu wake, mazunhumzo hao yalidumu kwa muda wa masaa mawili (2), ambapo Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan pia alihudhuria.
Mazungumzo hayo yanakuja huku kukiwa na “mkwamo” wa kisiasa visiwani humo baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, kuufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25, 2015 akisema ulijaa mizengwe na kadhia nyingi na kwamba tume itapanga tarehe nyingine ya uchaguzi.
Hata hivyo tangazo hilo lilipingwa kwa nguvu nyingi na maafisa wa CUF akiwemo Maalim Seif mwenyewe huku akisisitiza kuwa yeye ndiye msindi halali na kwamba mwenyekiti wa tume hiyo hana mamlaka ya kikatiba kufuta uchaguzi huo.
Baada ya mkwamo huo wa kisiasa kumekuwepo na juhudi mbalimbali za viongozi wa juu wakiwemo viongozi wa dini, kufanya vikao vya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo ambapo hata Rasi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein, amekwisha kutana mara kadhaa na Maalim Seif ingawa hakuna taarifa zozote zililokwishatolewa na viongozi hao wawili juu ya nini hasa walichokuwa wakizungumza ingawa wafuatiliaji wa mambo wamekuwa wakibashiri kuwa ni juu ya mkwamo huo wa kisiasa.
Mkutano huo wa Dkt. Magufuli na Maalim Seif unaelezwa kuwa ndio mkutano mkubwa na muhimu zaidi hadi sasa na kwamba suluhisho la mzozo huo sasa majawabu yako “jirani”. Baada ya mazungumzo yao, wakitumia diplomasia, waliwaambia waandishi wa habari kuwa mazungumzo yalikuwa mazuri na kwamba wote wawili wanaimani suala hilo litamalizika haraka




6 comments:
What the United Republic of Tanzania needs urgently now are broader political, legal, economic and social reforms that can open wide the window for the growth of true democracy based on more transparency, equality and freedom for the majority of Tanzania citizens, both in the Islands and on the Mainland. The war against corruption and public embezzlements cannot be waged successfully without tackling these fundamental sysmetic and structural issues. A new era of social,political and economic dispensation is required now and in order to be effective, it needs to be enshrined in a new broadly agreed upon national constitution that cannot be tampered with at the whims of selfish politicians. It is time for all leaders to put the national interests ahead of their individual or group interests.
Mh. Maalim Seif, kubwa Zaidi, ni kwanini uende peke yako kwenye mazungumzo hayo badala ya kuwa na mwakilishi wa upande wako hata mgombea mwenza wako?/ Tunategemea kutakuwa na muafaka wa aina gani na unaookubalika? ukiwa na mazungumzo mengine ni vyema uwe na muwakilishi pia! hili ni gumu na huwezi kushinda haya mambo wao wako wawili wewe mwenyewe>?????
Mchangiaji wa 5:03 ina maana wewe ndio hujui kiswahili? Na km hujui kiswahili uliwezaje mada mpk ukawa mchangiaji? Acha ubwege penda lugha yako mimi cjawahi ona wazungu wakiwa na ujinga km huu.... Pumbavu kabisa.
Maoni ya mchangiaji bamba moja hapo juu yametulia sana. Ila wewe mchangiaji namba tatu (1:31) ndiyo unaonekana mbumbumbu kabisaa, maana hata hicho Kiswahili unachozungumzia mbona kama kinakupiga chenga!! Sema tu labda lugha iliyotumika iko juu ya uwezo wako,ndiyo maana unatoka mapovu mazito pamoja na matusi na kama ni hivyo basi pole sana ndugu yangu. Hayo ndiyo matatizo ya kwenda shule za kata! Kama mtu akiamua kwamba anaweza kutoa hisia zake kwa ufasaha katika lugha ya kimombo kwenye jukwaa hili ni rukhusa, hakuna masharti kwamba lazima achangie kwa lugha ya Kiswahili. Kumbuka hili blogu ni la kimataifa na linasomwa na watu wengi, wajuzi wa Kiswahili na wengine ambao ni wanafunzi wa hiyo lugha au wapenzi tu na huenda hawaifahamu vyema. Usiwanyime wasomaji wa blogu hii fursa za kurutubisha akili na fikra!
Anonymous at 9.22: Well said; umesema ukweli; bien dicho.
Usituchafulie hali ya hewa hapa,kila mtu ana uhuru wa kuwakilisha mawazo yake kwa either kutumia kiswahili kama lugha ya taifa au kiingereza .lugha zote 2 zinaruhusiwa kwa mujibu wa katiba.ukitaka blogu za 100% uswahili zipo tele bongo..
Post a Comment