Baada ya Profesa Sospeter Muhongo kutangazwa kuwemo katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya awamu ya Tano lililotangazwa na Rais Dk. John P Magufuli, kumezuka maneno mengi katika mitandao na vijiwe vya siasa kukosoa uteuzi huo kwa kile kinachotajwa kuwa ni tuhuma zake za kuhusika katika sakata la Escrow ambapo alilazimika kujiuzuru.
Aidha, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, aliyekuwa anagombea urais kwa tiketi ya CHADEMA kwa kuungwa mkono na UKAWA alijiuzuru mwaka 2008 baada ya kutuhumiwa kuhusika katika sakata la Richmond.
Je, uwezo wa kulitumikia Taifa hili wa wawili hawa unapimwa kwa kipimo kipi? .... ni ufisadi .... ni kuwajibika kisiasa .... au ........Credit:Dar25

9 comments:
Hao wote wanao ukosoa uteuzi wa prof muhongo ilihali waliuunga mkono na kuusherekea uteuzi wa Edward Lowasa kama raisi wa Tanzania ni wanafiki na wazandiki wa hali ya ajabu kabisa.
profesa muhongo alijiuzulu sio kwa sababu alihusika. wakati escrow hela zikihizishwa Muhongo hakuwepo katika wizara hiyo wala wizara yoyote serikalini kama waziri. kilichotokea ni kwamba alijiuzului sababu kashfa imeihusisha wizara yake, amekuwa mstaarabu wa utumishi kama mzee mwiny alivyojiuzulu miaka ya sabini kutokana na kashfa ya mauaji yaliyofanywa na polisi yeye akiwa kama wazirii wa ulinzi. lowasa anajulikana alikuwa mpiga dili na mla rushwa. sasa kuwafananisha hawa wawili ni sawa kufananisha kifo na usingizi. tunajua ukawa wameshachoka sasa wanaanza pa kupatia kiki na wananchi wameshajua nini ni giza na ni nini ni mwanga. waache waongee sisi tunajenga nchi yetu
Prof. Muhongo hakuiba chochote
Sasa Lowasa anaingiaje tena hapa?? Huyo prof Muhongo alikuwemo kwenye kashfa ya ESCROW na walijichotea mabilioni na bosi wake lakini cha kushangaza kateuliwa tena kuwa waziri..nchi bado inaongozwa kutoka msoga!!!.hakuna cha spidi ya maguful wala cha kazi tu haha haaaa...
Maguful kachemsha kumteua mtu mwenye kashfa kama muhongo..kumbe ule moto wote aliokuwa nao ulikuwa moto wa mabua ..kubalini rais wenu kachemshaa!!!!
Sisi tunachosema "Mheshimiwa Muhongo karibu kundini" simamia katika kulinda gas yetu udalali wa gas hakuna..Hapa ni kazi tu..
nyie kubalini tu ni kwamba hafai...acheni kujigonga...angechagua mwingine maana mbegu zile zile
Prof. Muhongo has nothing to do with Escrow scandal but Lowassa was 100% involved in Richmond scandal and many other scandals. Lowassa ni mpiga deal.
UKAWA ARE BABY BOYS
Post a Comment