Wednesday, December 30, 2015

JK,WAZIRI LWENGE WAKAGUA MITAMBO YA MAJI WAMI,CHALINZE

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (katikati), akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete na Lwenge wakiangalia mitambo ya kusafisha maji.
Wakiwa katika picha ya pamoja
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete , akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge (kushoto kwake) wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.Wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akionesha kitu walipotembelea mitambo ya maji Wami

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge katika mitambo hiyo.

3 comments:

Anonymous said...

JK nadhani angepumzika tu kwa sasa msoga haya mambo ya kukagua miradi angewaachia wabunge na serikali ya magufuli pia Kama rais mstaafu haina picha nzuri kwa serikali ya sasa kuona rais mstaafu anakagua miradi.

Anonymous said...

JK alikuwa na nafasi & uwezo wa kuyafanya haya katika kipindi chake cha uongozi lakini he chose not to.Sioni ninini kinachomhangaisha sasa hivi.
Ni busara awaache waliopo sasa wafanyekazi kwa space,na mipangilio waliojiwekea.

Anonymous said...

YAANI NASHINDWA KABISA KUELEWA,KUIPATA LINK,ILIKUWAJE,NANA ALIMWALIKA KIKWETE,COVERAGE YAKE IMEKUA KUBWA KULIKO YA WAZIRI LWENGE.SIELEWI,SIELEWI,SIELEWI.SIASA ZA CCM KWELI UNAFIKI,MAJUNGU.KWA NINI MUNAMCHIMBA MHE.RAIS MAGUFULI?