
Magwiji hao wa Hispania wanaamini wanaweza wasimpate tena kocha mwenye hadhi wa kuchukua nafasi ya Rafa Benitez kama Mourinho atafanikiwa kumbadili Louis van Gaal pale Old Trafford.
Rais wa Real, Florentino Perez, ameiambia Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo kufanya kila liwezekanalo ili kumrejesha ‘Special One’ katika klabu hiyo yenye maskani yake, Santiago Bernabeu.
Ingawa mabosi wenzake ni kama wamegawanyika katika suala hilo, Perez ana wasiwasi hawatakuwa na upana wa kutosha wa kuchagua kocha pale watakapoamua kuachana na Benitez.
United imeshampanga Mourinho kwa ajili ya kuchukua nafasi watakapomtema Van Gaal na imeshahakikishiwa kwamba Mreno huyo yupo tayari kuipokea ofa ya kutoa Old Trafford.
Lakini kutokana na uchache makocha wa daraja la juu, Real ina wasiwasi wa kujikuta kwenye mazingira magumu itakapomtosa Benitez hasa kama isipowahi kumnasa Mourinho.
Benitez, kocha wa zamani wa Liverpool yupo kwenye hali ngumu kwenye klabu hiyo ya Hispania huku wachezaji wakizikosoa mbinu zake na namna anavyopanga kikosi.
Mashabiki nao wakimgeuka wakati Real ilipokuwa nyuma 2-1 kwa Rayo Vallecano, hata ilipobadili upepo katika mechi hiyo waliyoimaliza kwa ushindi wa mabao 10-2, bado kulikuwa na mawazo hasi kwake.
Perez na maofisa wengine wa Madrid wanafahamu kuwa Benitez hana mashiko katika chati za makocha mahiri na ingwa walimkingia kifua kocha wao wiki iliyopita, kuna tetesi kwamba anaweza kutimuliwa mwishoni mwa mwezi.
Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos ni wachezaji wenye ushawishi mkubwa klabuni hapo na wote hawafurahishwi na baaadhi ya maamuzi ya Benitez.
Wawili hao hawakupenda Carlo Ancelotti aondoke mwishoni mwa msimu uliopita na pia walikatishwa tamaa kuona anakubaliana na Bayern Munich wiki hii.
Huku Jurgen Klopp akiwa na Liverpool, Pep Guardiola akitajwa kuhamia Manchester City na Diego Simeone akiwa na wapinzani wao, Atletico, Mounrinho ndiye kocha pekee mahiri anayesalia kuweza kuchukua nafasi Real.
MWANASPOTI
No comments:
Post a Comment