ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 19, 2015

Kauli ya Mbowe baada ya MCC kuzuia Trilioni 1 kwa serikali ya Tanzania


Mwenyekiti wa Chama chadema, Freema Mbowe.
Muda mfupi baada ya Bodi ya MCC kutoa taarifa inayoonesha Tanzania haitapata msaada kutoka shirika hilo kama ilivyotarajiwa kwa ajili ya mwaka 2016, Mwenyekiti wa Chama Chadema, Freema Mbowe ametoa kauli nzito juu ya suala hilo akisema kuwa kuchelewa kupatikana kwa fedha za MCC si tu kunachafua jina la nchi na hadhi yake katika medani za kimataifa, bali kutaathiri kwa kiasi kikubwa miradi yote iliyo chini ya ufadhili wa MCC.
MCC imeahirisha msada huo wa USD Mil. 472.8 ambazo ni takriban trilioni moja kwa fedha za Tanzania zilizolengwa kusaidia sekta ya nishati ya umeme hususan ule wa vijijini, katika kuunganisha wateja wapya, mabadiliko ya kimuundo ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ili lifanye kazi na kutoa huduma kwa ufanisi katika sehemu za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji.

Fedha hizo pia zilikusudiwa kusaidia kuanza kwa mpango mkubwa wa kuboresha sekta ya umeme nchini.2014-2024.

Mbowe amemtaka Rais John Magufuli kuchukua hatua za haraka za kiuongozi kumaliza mtanziko wa kisiasa Zanzibar kwa mshindi wa nafasi ya urais kutangazwa kutokana na uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba, mwaka huu.

Aidha amesema kuwa Sheria ya makosa ya mtandao (Cyber Crime Act 2015) ambayo ni mojawapo ya sababu zilizotumiwa na MCC kuahirisha msaada huo kwa Tanzania hadi itakapokuwa imefanyiwa kazi, ni sheria mbaya sana inayokinzana na kukua kwa technologia ya habari na mawasiliano na kuzuia upashanaji wa habari miongoni mwa jamii ambayo ililenga kuweka makosa ya kijinai ili kudhibiti wapinzani wa CCM katika uchaguzi mkuu na kukipatia mazingira ya ushindi chama hicho.

“Sasa imethibitika kuwa Bodi ya MCC iliyokaa tarehe 16 Dec 2015 imeahirisha rasmi kuidhinisha msaada wa Millenium Challenge uliokuwa umekusudiwa kwa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2016. Sababu kuu mbili zilizosababisha uamuzi huo ni:

1. Mkwamo wa Uchaguzi wa Rais na Wawakilishi Zanzibar na
2.Matumizi mabaya ya she ria ya makosa ya mtandao hususan kuhusiana na uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa 2015.”

“Ubabe wa baadhi ya viongozi wa CCM ni janga la Taifa. Kuchelewa kupatikana kwa fedha za MCC si tu kunachafua jina la nchi na hadhi yake katika medani za kimataifa, bali kutaathiri kwa kiasi kikubwa miradi yote iliyo chini ya ufadhili wa MCC,” amesema Mwenyekiti Mbowe na kuongeza;

“Sheria ya makosa ya mtandao (Cyber Crime Act 2015) ni sheria mbaya sana inayokinzana na kukua kwa technologia ya habari na mawasiliano. Aidha, kwa makusudi kabisa inafifisha uhuru wa kupashana habari na ni dhahiri ilitungwa kwa nia mbaya ya kuthibiti kijinai uchaguzi mkuu.

“Tuliipinga sheria hii Bungeni na ikapitishwa usiku wa manane kwa ubabe wa wabunge wa CCM na hata tulipomtaka rais Kikwete asiisaini aliisaini kibabe akijua anaandaa mazingira gani ya “kihalifu”, “ amesema Mwenyekiti Mbowe.

Ameongeza kusema kuwa sheria hiyo ilitumika kuvamia vituo vya CHADEMA vilivyokuwa vikitumika kukusanya matokeo ya kura za rais na wabunge na hadi leo vijana zaidi ya 161, wakiwemo wanafunzi, wana kesi za “kubumba” mahakamani.

Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa Sheria hiyo hiyo ilitumika kuficha dhana ovu iliyotumika kuhalalisha kuvamia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilichokuwa kikiratibu watazamaji wa uchaguzi wa ndani kwa kibali cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Vile vile Sheria hii imetumika kuwakamata na kuwaweka ndani na hata kuwanyima dhamana vijana wetu ambao walituunga mkono katika uchaguzi mkuu.

“Namtaka rais Magufuli achukue hatua za kiuongozi na kiutawala kwa kufanya yafuatayo:

“Kwanza aumalize mgogoro wa kisiasa Zanzibar kwa kuhakikisha kuwa mshindi halali anatangazwa.

“Pili achukue hatua ya kuifanyia marekebisho makubwa Sheria ya makosa ya mtandao katika bunge lijalo. Aidha wale wote waliobambikiwa kesi amuamuru DPP kuzifuta kesi hizo mara moja,” amesema.

Mwenyekiti Mbowe amesisitiza kuwa Rais Magufuli hana budi kuchukua hatua hizo za haraka ili kulinusuru taifa na hasara ya kupoteza mabilioni hayo ya MCC na zaidi kuepusha kuporomoka zaidi kwa biashara ya utalii nchini Zanzibar.

Amesema katika taifa ambalo sekta ya umeme inakabiliwa na matatizo makubwa katika uzalishaji, usambazaji na usafirishaji huku wananchi wa kipato cha chini wakibebeshwa mzigo mkubwa wa kumudu nishati hiyo na wengine wakilazimika kutumia nishati mbadala kama mkaa unaotokana na miti hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira, serikali inayojua wajibu wake yenye viongozi wanaothamini uwajibikaji, haikupaswa kushindwa kuchukua hatua stahiki kutimiza vigezo vya msaada huo ambao umeshaisaidia Tanzania katika miradi mingine kadhaa.

Imetolewa Ijumaa, Desemba 18, 2015 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

7 comments:

Unknown said...

Well, Mr mbowe you need to be ashamed yourself. MCC not to provide the aids money to Tanzania for a certain reasons is one of their policy to the developing countries,obey me so i can help you. What the point crying for someone else money, it is their own money they can give us where and what ever they want. We are blessed with resourceful country why we can't make an effort having our own money abandoning with the foreign aids. What the sense of calling ourselves free country if we live depending on subsidies money? Mr mbowe as chairman of the opposition party what kind changes you're were campaigning to bring to the country if you're believing that only the aids money can run the country? Yes Tanzania as developing country need some help from friends of those the developed coutries but using the aids money to put pressure for the political means i don't think is the thing. Actually is the shame thing at the first place to be a nation of beggars. We are always saying that there is no something for nothing except there's will be always something for more things. No one can give you something without expecting something in return. Mr magufuli is on the right track on making the country economy strong so it can be run by itself. I believe MCC have their own goal by giving free aids money to Tanzania and it doesn't real matter what has been intended for but i also believe Tanzania as a free nation has its own goal due to its own national interest and doesn't real matter if aids money can be delivered or not. Luckily Tanzanians we have elected a Smart educated very patriotic leader he will real figure out what the best for country. What he needs is our 100% support so he can deliver it and i real believe on his watch Tanzania soon will need no more foreign aids money to run itself .Forget about Mbowe he is nothing. He real doesn't know what is doing or talking.If he was smart he wouldn't let Corrupted Lowasa running for the presidency of his party. He thinks Crying for the missing MCC aids money he is talking for something big, poor him. He failed to understand, it is the very shameful thing to do that as a leader. Encouraging the people to believe that if the country miss the aids we can't survive is the very serious mistake. Why mwalimu nyerere was fighting to death making sure no foreign aids is needed to the run country? Who's got better thinking of running the country between Mwalimu nyerere and Freeman Mbowe? If you think Mbowe got better ideas then don't work and wait for the foreign aid money to bring the power in your house, to build your school,to build your hospital, to build your road, to build for you a toilet cause we become the very lazy people for listening of the Mbowe type leaders until we can't even build our own toilets we are using the bushes to dump our waste thats why cholera will never go away. When salmin Amour was president of Zanzibar the foreign aids were cutting off for some time he never cry or licked some ones butt instead he fought back economical now tell me what the different of living between Zanzibar and Tanzania mainland where the aids were granted?

Anonymous said...

HUO NI MWANZO, KUNA UWEZEKANO WA MASHIRIKA NA MATAIFA MENGINE PIA KUFUATA NJIA HIYO KWA MISINGI YA KUITETEA DEMOKRASIA, NA TAYARI BAADHI YA NCHI ZIMESHAONYESHA DHAMIRA HIYO, SERIKALI YA JOHN POMBE MAGUFULI INAUWEZO WA KUTATUA MATATIZO HAYO HARAKA SANA KWA MASLAHI YA TAIFA NA WATANZANIA KWA UJUMLA. TUNAIOMBA SERKALI YA MAGUFULI KUWEKA UTANZANIA KWANZA

Anonymous said...

Ni shida kuwa na viongozi wa design hii ya akina Mbowe ambao mpaka leo wana mawazo ya kudhani nchi haiwezi kwenda bila kutegemea misaada.
Nilitegemea Mbowe angetumia fursa hii kuwa mobilize watu wa muungano mkono JPM katika austerity measures anazochukua,katika vita dhidi ya ufisadi na ukusanyaji kodi ili kuongeza revenue ya taifa.Wakati umefika kwa Taifa kuanza kujijengea uwezo wa ndani na kuwa na bajeti za maendeleo zisizo kuwa tegemezi kwa asilimia kubwa.
Tangu MMC program ilipoanzishwa mwaka 2004 ni nchi chache sana zimekuwa zikipokea msaada huo na nyingi miongoni mwa hizo ni maskini sana wasiokuwa na rasilimali kama sisi . Kama tuki manage resources zetu vema,hatupaswi kuwepo ndani ya kundi hilo.
Kumbuka " anaekupa cha bure kwa hiari, basi ana hiari ya kutokupa hata bila sababu za msingi".

Anonymous said...

KAFE MBELE NA U CUF WAKO.TUTATATUA MATATIZO YETU YA NDANI KWA KUTUMIA TARATIBU ZETU,KWA WAKATI WETU BILA KUINGILIWA AU KUSHINIKIZWA NA TAIFA LOLOTE LA NJE.
HIVI HUKO RWANDA,UGANDA ETC AMBAKO DEMOKRASIA ILISHAPINDA SIKU ZOTE WANAISHIJE!

Anonymous said...

I am just curious, what constitutional power does the President have in resolving the Zanzibar election issue? Isn't that up to the Zanzibar Electoral Commission assuming the body is bestowed with the power to independently oversee all electoral issues in the island? Regard the Cyber Act, if it was passed by the parliament and signed into law by the former president, shouldn't the issue be raised in parliament again or I am to assume that the President has the power to decree on such matters? Just trying to understand the Chairman's statement.
Thanks,

Anonymous said...

Hivi kweli siku hizi Tamzania imeishiwa viongozi wenye mtizamo chanya ama hata uelewa wa mambo! Ungedhani uzalenfo ungeviunganisha vyama vya kisiasa kutetea maslahi ya nchi yao! Uchaguzi wa Zanzibar bado wanaongea wenyewe. Hilo shirika lisilo la kiserikali lilokamatwa kuingilia uchaguzi ni washirika wa Wamarekani na kesi ipo mahakamani. Sasa wanataka nini zaidi? Hii ni kutafuta visingizi tu baada ya kuwa na vipaumbele vingi ambavyo vinaikabili Marekani kama vile vita huko Syria na penginepo.

Kama alivyosema Naibu Waziri wa Fedha tukikusanya mapato yetu vizuri hakuna shida ya kuwapigia wafadhili magoti. Tumuombee kheri Rais Magufuli na Serikali yake kwa uongozi mahiri.

Akina Mbowe vikaragosi vya watu wengine. Hawana jipya. Wasingeweza fanya hata robo ya anayoyafanya Magufuli. Mungu Ibariki Tanzania.

Anonymous said...

Bwana Mbowe kweli unatuaibisha for your poor reasoning. Tanzania ni Nchi huru, na hatuhitaji handouts from Foreign powers. Nchi yetu itasonga mbele bila the so-called MCC funds. Tusiruhusu Ukoloni Mambo Leo unaofanywa na Marekani, kupitia hili shirika la MCC la kutuweka sisi kama vibaraka wao. Mbowe akumbuke kuwa Tanzania inayo marafiki wengi ambao wanatupa misaada bila masharti. Tunamuomba Rais JPM afuate nyayo za hayati Mhe.Rais Nyerere, ambaye alikemea na kuwapuuza IMF miaka ya 70s kwa kujaribu kutuwekea nasharti (conditionalities) katika utoaji wa misaada ya maendeleo. Nyerere aliibuka mshindi na anaheshimika hadi leo duniani pote.