Monday, December 28, 2015

KUTANA NA MAJIBU YA NIYONZIMA BAADA YA YANGA KUMPIGA CHINI


Baada ya kumsimamisha kwa muda usiojulikana, hatimaye uongozi wa Yanga umetangza rasmi kuvunja mkataba na kiungo wake wa kimataifa kutoka Rwanda Haruna Niyonzima.

December 28, 2015, mkuu wa idara ya Habari wa klabu hiyo Jerry Muro, alizitaja sababu kubwa za klabu hiyo kufikia uamuzi huo.
“Mchezaji huyu amekuwa akichelewa na kukosekana mara kwa mara kwenye program za timu hususan anapokuwa amekwenda kwenye timu yake ya taifa ya Rwanda na pia kipindi ambacho mchezaji huyu amekuwa akienda likizo. Mara zote alipokuwa akiitwa na timu yake ya taifa amekuwa akiondoka bila kuomba ruhusa wala klabu kujua. Amekuwa akishiriki kwenye mashindano ambayo si rasmi na bila kuruhusiwa na klabu”, amesema Muro.

Mbali na kuvunja mkataba na Niyonzima, Muro ameeleza pia hatua zaidi zilizochukuliwa dhidi ya mchezaji huyo kipenzi cha wanajangwani.

“Klabu pia inamtaka Haruna Niyonzima kulipa fidia ya jumla ya dola za kimarekani 71, 175 hii ikiwa ni kufidia gharama ambazo Yanga imeingia katika kumuongezea mkata wake mpya ambao unamalizika mwaka 2017 “, aliongeza Muro.

Timu ya ushindi imepiga story na Niyonzima kutaka kujua hatma yake baada ya klabu yake kutangaza kuvunja mkata dhidi yake.

“Nimesikia tu kwa watu, lakini si sahihi kwasababu inavyotakiwa natakiwa kujua kupitia barua, lakini bado sijapata barua siwezi kulizungumzia hilo”, alisema Niyonzima wakati akizungumza na Hahaya Mohamed.

Mtandao huu haukuishia hapo tu, bali ulitaka kufahamu pia mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kutaka kujua wanamaoni gani baada ya klabu yao kutangaza imesitisha mkataba na Haruna Niyonzima.

“Niyonzima ni mchezaji mzuri, tulikuwa tunampenda lakini ana mambo yake hata sisi tulikuwa haturidhiki nayo. Kwasababu kama umeajiliwa lazima uitumikie kazi sasa wewe kama unaiona kazi haikufai basi tafuta sehemu nyingine”, alisema mmoja wa wanachama wakongwe wa klabu hiyo.

Awali klabu ya Yanga ilitanga kumsimamisha Haruna Niyonzima kwa kuchelewa kuripoti kambini baada ya kuitumikia timu yake ya taifa kwenye michuano ya Challenge Cup na kushindwa kutoa maelezo kwa kina baada ya kutakiwa kufanya hivyo.

Hapa chini unaweza kujionsea video wakati Niyonzima akitoa majibu yake alipoulizwa kama anataarifa juu ya kuvunjwa kwa mkataba kati yake na Yanga.




No comments: