ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 15, 2015

KUTANA NA WANANDOA WALIOTIMIZA MIAKA 90 YA NDOA YAO.


Hii inaweza kukushangaza kidogo, lakini ndiyo hivyo hutokea hasa pale mnapokubali kuaminiana na kupendana.
Mwenyezi Mungu kawajaalia kupata watoto 8, Wajukuu 27 pamoja na Vitukuu 23, wamefanikiwa mara kadhaa kukutana na Malkia wa Uingereza.

Wanandoa hao waishio nchini Uingereza wameadhimisha mwaka wa 90 wa ndoa yao.

Karam na Kartari Chand, wenye umri wa miaka 110 na mwingine 103, wanaaminika kuwa wanandoa waliokaa pamoja kwa muda mrefu zaidi nchini Uingereza.

Walifunga ndoa nchini India mwaka 1925, wakati binti akiwa na miaka kumi na mitatu. Wakahamia England miaka arobaini baadaye. Zawadi Machibya anasimulia.

No comments: