MBUNGE AFARIKI GHAFLA KWENYE KIKAO CHA BUNGE
Mbunge mmoja nchini Kuwait aliyetajwa kwa jina la Nabil Al-Fadl ameanguka ghafla na kupoteza maisha wakati kikao cha bunge kikiendelea.
Al-Fadl mwenye umri wa miaka 56 alionekana kwenye vipande vya video vilivyosambaa kwenye mitandao ya kijamii vikionesha akianguka kutoka kwenye kiti chake na kuanza kupewa huduma ya kwanza na waziri wa afya wa nchi hiyo, Dk. Ali Al Obaid hadi pale madaktari walipowasili lakini walishindwa kuokoa maisha yake.
Mbunge huyo alikuwa mwandishi wa habari machachari ambaye mara kadhaa aliwakosoa vikali wabunge wenzake na hata kuwakashfu. Alikuwa na wafuasi wengi waliokuwa wanamsapoti kutokana na misimamo yake ya kuikosoa serikali.
Alifahamika zaidi kwa kuwapinga vikali waasi wa kiislamu na kuwakaripia mara kadhaa alipopewa nafasi ya kuchangia bungeni na hata anapoandika kwenye gazeti lake.

3 comments:
ona wenzetu...waziri wa afya ni medical doctor siyo bongo eti waziri wa ulinzi ni medical doctor ...na waziri wa afya sijui ni vipi hapo
Siku nyingine andika kichwa cha habari hivi: mbunge afariki ghafla kwenye kikao cha bunge nchini Kuwait. Then andika story tunao ndugu kwenye bunge LA jamuhuri ya Tanzania hivyo mawazo yetu hayawezi kufikiria kama utatuandikia kufa kwa mbunge wa nchi nyingine.
Bongoland, anything goes!!
I am still waiting for the Chikawe, Mukangara et al to hand over their offices. The President, PM, VP all have done it, but I haven't seen any Minister doing so. Uchungu was kukosa uwaziri?
karibuni tule dagaa tena.
Post a Comment