Mbunge wa jimbo la Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea amefikishwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam mapema hii leo akielekea katika chumba cha kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Mbunge wa jimbo la Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea akiwa na wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo, leo mara baada ya kusomewa shitaka lililokuwa likimkabiri katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea akizungumza na waandishi wa habari katika mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake imeahirishwa hadi Desema 29, mwaka huu.Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
1 comment:
bwana kubenea punguza kutafuta umaarufu kwa kasi,utaumia,na utaharibu kazi.hivi vitu vinataratibu zake usikurupuke tu kisa mbunge!mkuu wa wilaya ni bosi wako,unahitaji kumsikiliza na kuelewana nae!kwanini hukuenda ofisini kwake na kupata muda mzuri wa kuchangia wazo lako kuhusu huo mgogolo?mwenzio kaanza nalo muda,wewe umekurupuka ulikotoka na kuleta usumbufu.makonda yuko sahihi
Post a Comment