Wednesday, December 9, 2015

MHE.BALOZI WILSON M. MASILINGI ATEMBELEA KITENGO CHA VISA KATIKA OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA, WASHINGTON D.C, SIKU YA KUMBUKUMBU YA UHURU, TAREHE 9 DISEMBA, 2015

Katika kutekeleza agizo la Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Ubalozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Washington D.C umendelea kufanya kazi na kutoa huduma za Visa na Pasipoti kama sehemu ya maadhimisho ya sikukuu hiyo.

Pamoja na kazi zingine za Ubalozi kuendelea kama kawaida, Mhe. Balozi Wilson M.Masilingi alitembelea kitengo cha Visa na huduma za Uhamiaji na kufanya mazungumzo mafupi na Mkuu wa Kitengo hicho Bw. Abbas A. Missana, Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi, (Minister Plenipotentiary).

Katika Mazungumzo hayo, Bw. Missana alimweleza Mhe. Balozi kuwa kumekuwa na ongezeko la wageni wanaokuja Ubalozini kuchukua Visa, mara baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 kumalizika salama. Hapo awali, kabla ya uchaguzi idadi ya wageni waliokuwa wanafika Ubalozini kuomba Visa ilipungua kwa kiasi kikubwa.

Mhe. Balozi aliwapongeza Wafanyakazi wa Ubalozi kwa kuitikia wito wa “Uhuru na Kazi” kwa hamasa kubwa, jambo linalodhihirisha uzalendo na kuheshimu miongozo sahihi toka kwa Mkuu wa Nchi na wasaidizi wake. Aidha, aliwataka Watumishi wa Ubalozi kuendelea kuboresha huduma kwa wateja ili kulinda heshima ya nchi yetu.

Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi (kulia) akipolewa na Bw. Abass Missana, Mkuu wa Kitengo cha Visa na huduma za Uhamiaji.

Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha Visa na huduma za Uhamiaji na wafanyakazi wa kitengo hicho. Kulia ni Bi. Swahiba H. Mndeme, Mkuu wa Utawala na Fedha, Ubalozini.

Mhe. Balozi Masilingi akisalimiana na Bi. Mariam Mkama, Mtumishi wa Ubalozi, kitengo cha Visa

Mhe. Balozi Masilingi akisalimiana na mmoja wa wateja wa Visa aliyefika Ubalozini kupata huduma hiyo
Mhe. Balozi Masilingi akizungumza na Bw. Arnold NzuaMtemi Nzali wa Las Vegas, Nevada aliyefika Ubalozini kupata huduma ya Pasipoti


4 comments:

Anonymous said...

Jamani, tuache siasa na usanii na tufanye kazi za kuwakilisha Watanzania inavayotakiwa. Hivi mnataka tuamini kwamba Mhe. Balozi alikuwa hajatembelea kitengo cha Uhamiaji ambacho kiko kwenye jengo moja la Ofisi ya Ubalozi, ghorofa ya chini ambapo yeye binafsi anapita kila siku kabla ya kupanda ofisini kwake tangu ashike wadhifa wa kuongoza ofisi hii zaidi ya miezi miwili iliyopita? Au alitaka tu kuonekana kwenye picha kutoa taswira ya kuunga mkono kauli mbiu ya "Hapa Kazi tu na Uhuru na Kazi" ya Rais JPM! Kwa stahili hii, basi tunaona mengi.

Anonymous said...

Jamani nani kawaambia kitengo hicho kipo jengo moja na ubalozi? Msilaumu bila kufahamu.

Anonymous said...

Nimepata habari za kwamba kitengo hicho kipo nje ya vitongoji vya washington dc

Anonymous said...

annony namba moja wacha roho mbaya. inaonyesha unapafahamu sana mahala hapo. fanya kazi yako wacha afanye yake. wewe mwenyewe ukipimwa unadhani utajaa