Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Takururu ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.
Bw Sefue amesema atakayekiuka agizo la rais "atachukuliwa hatua kali”.
Hii si mara ya kwanza kwa Dkt Magufuli kuwachukulia hatua maafisa wa Serikali tangu achukue madaraka mwezi uliopita. Siku chache baada ya kuingia afisini, a libadilisha usimamizi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kufanya ziara ya kushtukiza huko na kutoridhishwa na utoaji huduma

5 comments:
Inaonekana hawamuogopi Rais Magufuli, kama wanashindwa kutii maagizo ya rais hao wafanyakazi watatii maagizo ya mtu yeyote yule? Wamenyimwa kibali cha kusafiri lakini wamesafiri......kuna nini kwenye hizo safari hadi wafanyakazi washindwe kujali amri ya rais ambaye ni bosi wao? Halafu wamenyimwa....kama wasingeomba si wangekwenda kienyeji bila kutoa taarifa? Wafanyakazi wa serikali yetu hawana nidhamu kabisa!! Kama hawamheshimu rais wa nchi ambaye ndiye bosi wao mkuu je watawaheshimu wananchi wanaohitaji huduma?? Udhaifu huu wa serikali unaonekana na hata mtoto mdogo anauona, hao wafanyakazi wamefanya kinyume cha sheria kwa makusudi walipaswa wafukuzwe(summary dismissal), lakini eti wanasimamishwa???? Kwanini wasifukuzwe na uchunguzi kufanywa kwanini walipuuza amri ya mwajiri wao???? SERIKALI MNAJIDHARAULISHA WENYEWE.
Hao watumishi waliosafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha kusafiri wanatakiwa wachunguzwe kwa makini! Safari hiyo siyo bure kuna kitu kinachoendelea kwenye hiyo taasisi ya umma! Yasiwe Yale mambo yakwenda Kuweka sawa / Kuficha Mapesa!
How on earth can you do that? Hive vibali vya Ikulu si sawa na wakati wa Nyerere, we used to apply for State House Clearances.
Wamesimamishwa, nchi zingine you are sacked if you don't obey orders from the Top.
JEE SERIKALI INAJUA KUWA GHARAMA ZA KUMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI NI KUBWA MNO.KAKUTWA NA KOSA,TENA KUBWA UNAMSIMAMISHA KAZI BADALA YA KUMFUKUZA.MTINDO HUU MBAYA ULIOANZA MWISHO WA SIKU UTAKUTA MAELFU WAMESIMAMISHWA KAZI,MAELFU WAMEREJESHWA KAZINI NA IMEAMRIWA WALIPWE MABILLION,HASARA JUU YA HASARA AINA HII YA UONGOZI INA KASORO,HUSUSANI WEWE BALOZI OMBENI SIFUE,HAPO HUPAWEZI,UONDOLEWE,UONDOKE.
Sijakubaliana na mtoa hoja ya katibu Mkuu aondoke , huyo bwana yuko makini sana ktk kazi yake na anamfaa sana Rais wetu kwa Wakati huu.
Post a Comment