Wednesday, December 9, 2015

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI ZOEZI LA USAFI SOKO KUU LA CHALINZE

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Welle Ndikilo wakielekea soko kuu la Chalinze kushirikiana na wananchi kufanya usafi wa mazingira leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakifanya usafi katika soko kuu la Chalinze leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na wananchi wa Chalinze baada ya kushirikiana nao kufanya usafi wa mazingira ya soko kuu la Chalinze leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli

7 comments:

Anonymous said...

Asante miaka kumi yote ulikuwa hulioni hilo. Kusafiri nchi za wenzetu ukaona usagi wa miji na barabara taa zikiwaka usiku, taa za barabarani kama maua umeme usiokatika marakwa mara ulidhania zilikuwepo bila mbinu na mkakati! Hebu toa fedha uliyojilimbikizia tufanye kazi mkuu wetu na kijana pia..

Anonymous said...

HAPA KAZI TU.

Anonymous said...

Fyuuu
angefagia mafisadi aliyowaleya miaka 10
Afagiye leo kisa kutuletea TB
Mtu mzima ovyo

Anonymous said...

hawa nao utazani ma super star hawapumziki huko bwagamoyo wakala upepo kimya kimya?

Anonymous said...

Usafi bila glove na ana viatu vya kutokea,huyu jamaa bonge la msanii

Anonymous said...

KIBAYA ZAIDI BAADA YA SHUGHULI ZA USAFI ALIHUTUBIA.ALISEMA HAJAWAHI KUMSAMEHE MFANYA BIASHARA KODI,AKAITETEA PIA FAMILI YAKE.ANACHOKOZA HASIRA ZA WANANCHI.UNAJUA SASA HIVI DOLA IENDELEE KUORODHESHA MAKOSA YAKE YA KIJINAI NA MATUMIZI MABAYA YA OFISI,WAKATI HUO HUO MWANASHERIA MKUU AENDELEE KUUANDAA MUSWADA WA KUFUTA KINGA YA KUTOKUSHITAKIWA,ILI VIKISHAPITISHWA NA BUNGE LETU WANANCHI WASHUHUDIE KUPITIA MAHAKAMA ZETU USHAHIDI UNAOONYESHA MATRILLION YALIVYOLIWA NA WACHACHE WAKATI WA UTAWALA WA AWAMU YA NNE.INATISHA.INAOGOFYA.WIZI BALAA,KUJINUFAISHA BALAA,HAIJAPATA KUTOKEA.

Anonymous said...

jamani, jamani, jamani,mbona muda wa kukanusha bado.Sasa hivi bado kabisa vinakusanywa mashtaka na ushahidi,serikali ikichelewa basi taasisi kadhaa zilizosheheni ushahidi wa wizi na matumizi mabaya ya ofisi zitapanga foleni mahakamani.mimi nayaona yale yale ya marehemu rais mstaafu wa zambia Chiluba yanakuja Tanzania hivi karibuni.