Mkurugenzi wa barabara Wizara ya
Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Ven Ndiyakumana kushoto
akisaini mkataba wa awali kuhusu mkopo wa fedha wa riba nafuu
utakaosaidia ujenzi wa Barabara ya Arusha hadi Holili kulia ni Naibu
Mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano Afrika kutoka Japan (JICA) Bw.
Hideyuki Manioka wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi wa barabara Wizara ya
Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Ven Ndiyakumana kushoto
akikabidhiana mkataba wa awali kuhusu mkopo wa fedha wa riba nafuu
utakaosaidia ujenzi wa Barabara ya Arusha hadi Holili na Naibu
Mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano Afrika kutoka Japan (JICA) Bw.
Hideyuki Manioka wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Jijini Dar es
salaam.PICHA ZOTE NA ALLY DAUD-MAELEZO
Na Raymond Mushumbusi Maelezo
Serikali ya Tanzania kupitia
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano leo imesaini mkataba wa
makubaliano ya awali ya ujenzi wa barabara kutoka Arusha mpaka Holili.
Makubaliano hayo yamesainiwa na
Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Ven Ndyamukama kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Naibu
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano (JICA) Bw Hideyuki Manioka kwa niaba ya
Serikali ya Japan.
Mhandisi Ven Ndyamukama amesema
kuwa Tanzania imesaini mkataba huu wa awali ambao baada ya majadiliano
ya awali kati ya Tanzania na Japan, serikali ya Japan itatoa mkopo wa
riba nafuu kwa serikali ya Tanzania ili kuwezesha kuanza kwa utekelezaji
wa mradi huu mapema marchi mwakani.
“Wamekuja kufanya utafiti na
kufatilia taarifa tulizo nazo kuhusu mradi huu na kupeleka taarifa
serikali ya Japan na tunategemea June mwakani kusaini hati ya kupata
mkopo ambao utawezesha ujenzi wa barabara hii ” Alisema Mhandisi
Ndyamukama.Pia ameongeza kuwa baada ya
mkopo huo kutolewa wao kwa upande wao wamejipanga katika kufanya mradi
huo ukamilike kwa wakati ikiwemo upatikanaji wa wakandarasi kwa ajili ya
mradi huo.
Aidha Naibu Mkurugenzi wa Idara
ya Ushirikiano (JICA) Bw Hideyuki Manioka amesema kuwa wataendelea
kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kusaidia miradi mbalimbali
ya maendeleo.
Mradi huu wa barabara toka
Arusha mpaka Holili yenye urefu wa kilometa105 umefadhiliwa na Serikali
ya Japan kupitia Wakala wa mambo ya Ujenzi(JICA) na unatarajiwa kuanza
mapema mwakani,hii ikiwa ni juhudi za Serikali katika kuboresha
miundombinu hasa ya barabara kwa kuzifanya barabara nyingi nchini kuwa
katika kiwango cha lami.
No comments:
Post a Comment