ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 2, 2015

Tanroads yaanza ujenzi barabara ya Mwenge hadi Morocco Dar.


Mkurugenzi Mtendaji wa Tanroads, Patrick Mfugale.


Wakala wa Barabara Tanzania ( Tanroads), uameanza utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli kwa kufanya hatua za awali wa ujenzi wa barabara ya Mwenge Morocco katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Shughuli za upanuzi ya zilizoanza jana zilikuwa ni kusawazisha udongo na kuondoa baadhi ya mabango yaliyopo ndani ya eneo itakayopita barabara hiyo.

Nipashe jana lilifanya ziara katika barabara hiyo na kushuhudia ‘katapila’ mbili zikiendelea na usawazishaji kuanzia kilichokukwa Kituo cha Daladala Mwenge hadi Kituo cha Daladala cha itv.

Baadhi ya mafundi waliohojiwa kwa masharti ya kutotajwa majina yao gezetini kwa madai si wasemaji, walisema walianza hatua hizo za awali za ujenzi asubuhi huku wakisisitiza upanuzi wa barabara hiyo hautachukua zaidi ya miezi miwili.


“Tumeanza usawazishaji asubuhi eneo hili kama unavyoona mabango yaliyopo upande huu mmoja yameondolewa na nyasi zimekusanywa upanuzi huu hautazidi zaidi ya miezi miwili,” walisema.

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa Tanroads, Aisha Malima, alisema ujenzi huo umeanza upande mmoja wa barabara hiyo kwa kukata miti na kuondoa udongo wa juu.

“Ujenzi umeanzia Mwenge mkandarasi ameanza kwa kukata miti na kuondoa udongo,” alisema Malima.

Aliwataka watembea kwa miguu na madereva kuwa wavumilivu na kutoa ushirikiano katika kipindi hiki cha ujenzi.

Alipotafutwa kupitia simu ya mkononi, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanroads, Patrick Mfugale, kuzungumzia suala la ujenzi wa barabara hiyo alipokea na kujibu yupo katika kikao na kwamba atapiga atakapomaliza atapiga simu kuitolea ufafanuzi.
CHANZO: NIPASHE

1 comment:

Anonymous said...

Hili ni wazo tuu kuhusu ujenzi wa barabara, kupunguza msongamano/traffic kwa saa za asubuhi , wajenzi mngefanya kazi hiyo usiku na siku za weekend kama wenzetu wa makampuni ya hapa marekani wanavyofanya.. sasa hiyo inahitaji nguvu kazi ya kiukweli siyo legelege ya vibarua wa hapa tanzania ambaye ameamka na uchovu wa pombe ya gongo .