ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 11, 2015

Tanzania yapata maabara ya kipekee


Image captionTanzania na Nigeria ndizo nchi pekee zenye maabara ya aina hiyo Afrika kusini mwa jangwa la Sahara
Tanzania ni moja kati ya nchi zilizofanikiwa duniani kuratibu maabara inayohamishika kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ebola na magonjwa mengineyo ya mlipuko.
Maabara hii inaweza kusafirishwa mpaka kwenye maeneo yaliyoathirika, ikiwa ndani ya masanduku yaliyofungwa vyema badala ya kusafirisha sampuli kwa ajili ya vipimo kutoka eneo moja kwenda jingine na kuwa katika hatari ya kuathiriwa na vijidudu vingine.

Tanzania na Nigeria ndizo nchi pekee kusini mwa Jangwa la Sahara zenye maabara ya aina hii ambayo itakuwa msaada mkubwa pia kwa nchi za jirani za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR Dokta Mwele Malecela, amesema maabara hii ina umuhimu kwa kuwa itawezesha kufanyika kwa uchunguzi kwa urahisi na haraka zaidi, hata katika maeneo yaliyo na ugumu kufikiwa.Image captionMaabara hiyo inatarajiwa kurahisisha uchunguzi wa magonjwa hatari

Changamoto ambayo ilionekana wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi ni wahudumu kutofika kwa urahisi kwenye maabara kwa ajili ya uchunguzi wa haraka kutokana na umbali na miundo mbinu mibovu.

2 comments:

Anonymous said...

Hii wongo mtupu. Afrika Kusini zipo kadhaa. jamani ukweli siku hizi umekuwa mzigo

Anonymous said...

Tanzania kwa propaganda tunaongoza! Maabara ya dollar laki mbili ($ 200,000) ndiyo mnasema haipo Africa Mashariki na kusini? Hizo zipo nyingi sana hata hapo Kenya, dollar laki mbili tu hata nyumba aliyonunua waziri wa zamani ni ghali kuliko hiyo maabara yenu feki....halafu mnasema hiyo ni State of Art laboratory, muwe wakweli acheni propaganda rahisi, pia fanyeni research kwanza kabla ya kukurupuka tu, maabara za namna hiyo zimejaa kila mahali na wala hazina jipya.