Msemaji wa Simba, Haji Manara
Katika kuhakikisha hakuna senti tano ya kodi inayopotea, Mamlala ya Mapato Tanzania (TRA) imetinga ofisi za Simba na kukagua mahesabu ya klabu hiyo na kutoa mwongozo unaotakiwa kuanza kutekelezwa mapema mwezi ujao.
Mwongozo huo ni pamoja na kuhakikisha klabu inalipa kodi kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha wote wanaolipwa mishahara wanakatwa kodi.
Msemaji wa Simba, Haji Manara alisema jana kuwa TRA walifika kwenye ofisi za klabu hiyo kwa lengo la kufanya ukaguzi wenye lengo la kujua mapato ya klabu hiyo.
Alisema maofisa wa TRA waliridhika na taratibu za mahesabu ndani ya klabu hiyo.
“Ukaguzi wao hawakukuta shaka, mahesabu yetu yanakwenda vizuri. Walipata ushirikiano wa kutosha kutoka idara ya uhasibu ya klabu,” alisema Manara.
Hata hivyo, alisema TRA imewataka kuanzia Januari mwakani wahakikishe wanasimamia vizuri ulipaji wa kodi kulingana na mapato ya klabu.
Alisema mwongozo huo wa TRA unawataka kuhakikisha wale wote wanaposawa kulipa kodi kwa mujibu wa sheriwa wanafanya hivyo.
“Wachezaji na wengine wanaopaswa kulipa kodi kwenye klabu lazima wafanye hivyo. Huu ndiyo mwangozo yuliopewa na kutakiwa kuanza kuutekeleza Januari mwakani,” alisema msemaji huyo. Ukaguzi kama huo pia unafanyika Yanga, ingawa mhasibu wa klabu hiyo, Baraka Deusdedit alisema kinachoendelea hivi sasa ni vikao vya ndani na maofisa wa TRA kuhusiana na ulipaji kodi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Deusdedit alisema wako kwenye mazungumzo na TRA kuhusiana na suala zima la ulipaji kodi, ikijumuishwa mishahara ya wachezaji na makocha.
“Ni kweli, tuko kwenye mazungumzo na TRA kwa sasa ni mapema kusema hadharani tulipofikia, lakini itoshe kusema kwamba tunaendelea vziuri,” alisema Deusdedit.
Alisema, awali TFF ndio walikuwa wakilipa kodi hizo kupitia mapato ya uwanjani, lakini kwa sasa suala hilo limerejeshwa mikononi mwa klabu.
Tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya tano, suala la ulipaji kodi limekuwa mjadala mkubwa kutokana na msimamo uliopweka na serikali.
Tayari TRA imezizuia akaunti za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kile kilichoelezwa kukwepa kulipa kodi inayofikia Sh. bilioni 1.6.
Kutokana na kuzuia kwa akaunti hizo, TFF imefuta mkutano wake mkuu wa mwaka uliopangwa kufanyika jijini Tanga mwezi huu, lakini pia ikisema kama hakutakuwa na maafikiano na TRA Ligi Kuu inaweza kushindwa kuendelea mzunguko wa pili.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment