Wednesday, December 9, 2015

UZINDUZI WA FILAMU YA ‘GOING BONGO’ KUFANYIKA SIKU YA IJUMAA KWENYE UKUMBI WA SINEMA WA MLIMANI CITY

FILAMU mpya inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ ambayo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa filamu ndani na na nje ya nchi  imekamilika  sasa kuzinduziliwa rasmi siku ya  Ijumaa kwenye ukumbi wa sinema wa Century Cinemax uliopo Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi huo mtunzi na muandishi ambaye pia ameisimamia  katika kuitengeneza na kuigiza filamu hiyo, Ernest Napoleon alisema, “Naamini kuonyeshwa kwa filamu hii kutaandika historia muhimu kwenye tasnia ya filamu  nchini Tanzania”
“Tunashukuru kupata  nafasi hii kwani tunategemea tutaweza kubadilisha utamaduni wa kuangalia filamu haswa pale filamu nyingi za hapa nyumbani zikipana nafasi ya kuonyeshwa kwenye majumba ya majumba ya sinema” alisema.
Filamu hiyo ambayo mpaka sasa imetwaa tunzo kadhaa, ina maudhui ambayo yanonyesha maisha ya Daktari aliyejitolea kwenda kufanya huduma  nchini Tanzania kwa muda wa  mwezi mmoja.
Filamu hii imerekodiwa   majiji makubwa mawili ambayo ni Dar es Salaam na California  Marekani, inaelezea sehemu ya maisha ya kweli aliyonayo Daktari  mwenye asili ya nchini Ufaransa  aliyeondoka Ulaya na kwenda kufanya kazi  barani Afrika.
Kati ya tuzo ambazo filamu hii imeshinda ni pamoja na, Filamu Bora Afrika Mashiriki katika tamasha la Zanzibar International Film Festival (Ziff)  na Filamu Bora ya Kimataifa katika tamasha la ‘Black Entertainment Fashion’,  ‘Film and Television Awards’  (BEFTA)
Amewaomba mashabikmi wa filamu kujitokeza kwa wingi kesho kwenye uzinduzi huo ambapo tiketi zimeshaanza kuuzwa Century Cinemax Theaters Mlimani City.

No comments: