Thursday, December 10, 2015

WANAFUNZI WA CHUO CHA KODI JIJINI DAR WATIMIZA WAJIBU KUFANYA USAFI KATIKA CHUO CHAO

Afisa Mahusiano wa Chuo cha Kodi cha Mamlaka ya cha Mwenge jijini Dar es Salaam, Rahel Mkundai akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na siku yo ilikuwa ni kusherekea siku ya uhuru na kutumia siku hii kwa kufanya usafi wa mazingira.

CHUO cha Kodi cha Mwenge jijini Dar es Salam wameitikia wito wa kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kufanya usafi katika mazingira ya Chuo hicho.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kodi, Edward Mwakimonga amewasihi wanafunzi pamoja na wananchi kuwa usafi ni afya na ikiwezekana iwe ni kawaida kufanya usafi katika mazingira ikiwezekana baada ya wiki mara moja ili kuweka mazingira safi.

Nae Waziri Mkuu wa serikali ya chuo cha Kodi, Jeremia Shushu amewashukuru wanafunzi pamoja na menejimenti ya chuo hicho kwa kukubali na kujitokeza kwa wingi kushirikiana kufanya usafi katika mazingira ya chuo chao.
Wanafunzi wa chuo cha Kodi wakishirikiana bega kwa bega kufanya usafi katika chuo chaoo leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni kusherekea sikukuu ya Uhuru Desemba 9.Wanafunzi wakizoa takataka.
Wanafunzi wa chuo cha Kodi wakilima maeneo yenye majani.
Mwanafunzi wa chuo cha Kodi akitoa majani yaliyofyekwa
Wanafunzi wa Chuo cha Kodi cha jijini Dar es Salaam wakitupa takataka katika dampo.
Takataka zikiteketezwa.
Wanafunzi wakipruni mti.
Waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Kodi, Mwenge jijini Dar es Salaam, Jeremia Shushu akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kufanya usafi katika chuo chao akiwashukuru wanafunzi wa chuo hicho kwa kujitokeza kufanya usafi katika chuo hicho.

No comments: