MBUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), tawi la Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mh. Eugen Kaihura, ofisini kwa Balozi, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Jumatano Januari 13, 2016.
Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wao, Mh. Bhanji alsiema, Rwanda ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ilivyo kwa Tanzania, na Bunge la Afrika Mashariki linaundwa na wabunge kutoka nchi zote wanachama ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda, hivyo aliona umuhimu wa kwenda kumtakia heri ya mwaka mpya balozi huyo wa Rwanda.
Naye Balozi wa Rwanfa hapa nchini, Mh. Kaihura, alimshukuru mbunge huyo kwa kumtembelea ofisini kwake na kumtakia heri ya mwaka mpya, na kumuhakikishia Rwanda ambayo ni mwanachama wa Jumuiya itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa jumuiya hiyo ili kujenga Afrika Mashariki iliyo na ustawi wa hali ya juu na ushirikiano uliotukuka
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mh. Shy-Rose Bhanji, (kushoto), akipeana mikono na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mh.Eugene Kayihura ofisini kwa balozi Masaki jijini Dar es Salaam, Jumatano Januari 13, 2016. Mh. Bhanji alifika kumsalimia na kumtakia heri ya mwaka mpya balozi huyo ambaye nchi yake ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, (kushoto), akiwa na mazungumzo na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mh. Eugen Kaihura kwenye ofisi ya Balozi, Masaki jijini Dar es Salaam Jumatamo Januari 13, 2016. Mh. Bhanji alifika kumsalimia na kumtakia heri ya mwaka mpya balozi huyo ambaye nchi yake ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mh. Bhanji akizungumza na waandishi wa habari
Mh. Bhanji na balozi Mh. Kaihura wakiwa kwenye mazungumzo
Mh. Balozi Kaihura akizungumza na waandishi wa habari
Mh. Bhanji akiweka saini kitabu cha wageni ofisini kwa balozi Kaihura
Mh. Balozi Kaihura akimsindikiza mgeni wake Mh. Bhanji
Mh. Balozi Kaihura, akimuonyesha umbo la kitamaduni lililobuniwa nchini Rwanda likionyesha rangi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
No comments:
Post a Comment