Saturday, January 16, 2016

BREAKING NEWS: CHADEMA YANYAKUWA KITI CHA MEYA WA KINONDONI, NI BONIFACE JACOB

Diwani wa Kata ya Ubungo, Boniface Jacob akishangilia mara baada ya kushinda kwa nafasi ya Umeya wa Kinondoni kwa kupata kura 38, mapema leo Januari 16.2016, dhidi ya mpinzani wake, Benjamini Sitta aliyepata kura 20, dhidi ya kura zote zilizopigwa 58 katika Manispaa hiyo ya Kinondoni. (Picha na Andrew Chale).

Na Andrew Chale
Tayari kitandawili cha Umeya wa Manispaa wa Kinondoni kimesha teguliwa ambapo Meya mpya kwa sasa ni Boniface Jacob ambaye anachukua nafasi hiyo muda mfuoi kutoka sasa baada ya kushinda kwa kura 38 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kura 20, ambaye ni Benjamini Sitta kutoka CCM.
Wajumbe halali waliopiga kura katika baraza hilo la kumchagua Meya walikuwa 58, ambapo 38 ni kutoka Umoja wa vyama vya UKAWA huku upande wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wao wakiwa 20.
Hata hivyo uchaguzi huo uliokuwa wa huru na haki kwa pande zote, kura zilizipigwa kwa uwazi kwa pande zote. Aidha baada ya ushindi huo, upande wa kura za Unaibu Meya nafasi hiyo ilienda kwa mgombea wa CUF ambaye ni Jumanne Amiri Bunju ambaye yeye alipata kura 38 huku mpinzani wake kutoka CCM Diwani Manyama akiambulia kura 27 huku kura moja ikiharibika.

CHANZO: MODEWJI BLOG

2 comments:

Anonymous said...

Mmesema wapiga kula walikuwa 58. Sasa hiyo nafasi ya naibu meya imekuwaje ipigiwe kura na watu zaidi? 38+27+1=66. 66-58= 8. So hizo 8 zaidi zimetokea wapi au ndio bao la mkono? Lol!

Anonymous said...

Mmesema wapiga kula walikuwa 58. Sasa hiyo nafasi ya naibu meya imekuwaje ipigiwe kura na watu zaidi? 38+27+1=66. 66-58= 8. So hizo 8 zaidi zimetokea wapi au ndio bao la mkono ikashindikana? Lol!