
Akitoa taarifa hiyo jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema kuwa Mtweve ameteuliwa kuwa katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Balozi Sefue alisema Chagonja ameteuliwa kuwa katibu tawala wa Mkoa wa Katavi ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Sefue alisema Dk Magufuli ameamua kuwateua makamishna hao wa Polisi kama alivyowateua majenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuwa makatibu wakuu wa wizara, kwa lengo la kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.
Mtweve na Chagonja pamoja na Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini Kuwait, wataapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment