Dar es Salaam. Operesheni ya kukamata raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini bila ya kuwa na vibali imebaini China na Burundi zinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji haramu ikilinganishwa na nchi nyingine.
Tangu kuanza kwa operesheni hiyo nchini Desemba 8, mwaka jana hadi Januari 14, mwaka huu, idadi ya raia wa kigeni wasiokuwa na vibali waliokamatwa kutoka China walikuwa ni 285, Burundi 284, wakifuatia 157 wa Ethiopia.
Raia wengine waliokamatwa ni kutoka India 41, Zambia 40, DRC 34, Malawi 27, Kenya 26, Uganda 13, Ivory Coast 10, Korea tisa, Nigeria wanane, Somalia saba, Madagascar watano, Rwanda watatu, Lebanon, Zimbabwe, Ghana na Afrika Kusini mmoja kila moja na wengine 11 uraia wao ni wa utata.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza katika mwaka mpya wa China Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, alisema: “Kati ya hawa, baadhi wamepelekwa katika kambi za wakimbizi, hasa raia waliotoka Burundi, wengine wamepewa amri ya kuondoka nchini na wengine kesi zao ziko katika hatua mbalimbali mahakamani.”
Kitwanga alibainisha kuwa operesheni hiyo ya kukamata raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini bila vibali haitawagusa wenye vibali halali.
Kitwanga alisema wizara yake imetoa vibali vya ukazi kwa wageni 40,765 kutoka mataifa mbalimbali kati ya mwaka 2014 na Januari mwaka huu na kwamba idadi hiyo inaendelea kuongezeka siku hadi siku.
“Wageni waliofukuzwa kwa sababu mbalimbali mwaka 2015 ni 1,642,” alisema.
2 comments:
Warudishweee Makwao haraka Sanaa!!! Wamefanya Tanzania choo !! China ukizamia wakikubambaaa unafungwa kabisaa na wnakugongea muhuri hutaka uingie nchini Kwao tenaaaaaa!! Sasa iwajeee wao wafanye TZ choo cha kuingia tu?? Tanzania imekuwa haithaminiki wala kuheshimika na hao wahamiaji haramu!! Na wanao waajiri wapigwe faini ya mamillioni ili wakomeeeeee kabisaaaa kuwaajiriii!!!
Jamani kila nchi duniani ina wahamiaji haramu sio Tanzania tu. Wachina wanachoharibu ni kutengeneza viwanda feki ndani ya nakazi yao na kuwauzia wananchi bidhaa zisizo na viwango vya tbs.
Post a Comment