Saturday, January 2, 2016

EDDAH ELEGANT CATAERING YAMFANYIA GEOFREY KINYASHI MNUSO WA NGUVU WA MIAKA 50 YA KUZALIWA

Geofrey Kinyashi na mkewe Maria wakipata picha ya kumbukumbu baada ya Maria alipoishirikisha Eddah Elegant Catering na kumfanyia mumewe sherehe ya miaka 50 ya kuzaliwa iliyokua siri kwa mwaka mzima bila mume kujua na kukutana na surprise siku ya Ijumaa January 1, 2016 ilipofanyikia The Signature Blue Beltsville, Maryland nchini Marekani.
Geofrey Kinyashi akiwa na mkewe meza kuu.
Watoto Francis na William (kulia) wakiwa na marafiki zao kwenye meza kuu na baba na mama yao kwenye sherehe ya kuzaliwa ya miaka 50 ya mzazi wao.
Marafiki waliosoma na Geofrey Kinyashi tangia Sunday school, shule ya msingi na sekondari kutoka kushoto ni Duncan Silayo, Mariam Kalala Nyang'oro na William Kibaja wakiongea jinsi walivyomfahamu Birthday Boy enzi hizo. Duncan na William wanatokea jimbo la Massachusetts na Mariam anatokea jimbo la North Carolina.
Francis Kinyashi akimtakia baba yake kheri ya siku ya kuzaliwa huku mdogo wake William akifurahia anachoongea na baadae nae alimtakia baba yake kheri ya siku ya kuzaliwa.
Baba na mama Kinyashi wakifarahia jambo, kushoto Vero mdogo wa Maria aliyekuja toka jimbo la Georgia kwenye sherehe ya miaka 50 ya siku ya kuzaliwa ya Geofrey Kinyashi siku ya Ijumaa January 1, 2016 ilipofanyikia The Signature Blue Beltsville, Maryland nchini Marekani.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi.
Eddah Elegant Catering wakifungua mvinyo na kuwawekea kwenye glasi zao Geofrey Kinyashi na mkwewe wakiwemo marafiki wanafunzi wenzake. Mwenye koti la bluu kati ni Pendo Nyang'oro, mume wa Mariam.
Wakigonganisha glasi.
Wakinywa kwa afya na kusherehekea miaka 50 ya Birthday Boy.
Maria akimlisha keki mumewe.
Geofrey akimlisha keki mkewe.
Geofrey akimlisha keki mwanae Francis.
Geofrey akimlisha keki mwanae William.
ni mduara ukiendelea.

No comments: