Picha na Maktaba
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari Ijumaa hii, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya maandilizi ya shindano hilo Juma Pinto, amedai kuwa sababu ya kujitoa kwenye kamati hiyo ni kutokana na kushindwa kujua nini majukumu yao na yale ya kampuni inayoyaanda, Lino Agency.
Amedai kuwa awali iliwekwa wazi kuwa ni kamati hiyo ndiyo itakayoratibu mashindano hayo huku Lino Agency ikibaki kuwa washauri.
Pinto amesema Lino imeendelea kufanya kazi yake lakini wao wakibaki bila kujua kinachoendelea. “Sisi tumeona tuje tuzungumze tu kwamba sisi hatupo huko,” amesema Pinto.
Naye msemaji wa kamati hiyo, Jokate Mwegelo amesema kutokana na ukubwa wa kile Miss Tanzania imefanya kwa wasichana, wasilichukulie kwa wepesi na kiubinafsi.
“Waangalie wasichana wa Tanzania wanawatoaje? Na kuwatoa ni kuhakikisha kwanza misingi ya shindano lenyewe iwe ya kueleweka. Kama misingi haieleweki ndio tunarudi kule kule,” amesema Jokate.
Aliongeza kuwa makosa yaliyojitokeza miaka iliyopita pamoja na malalamiko mengi dhidi ya shindano hilo yanapaswa kufanyiwa kazi.
Kamati hiyo ya Miss Tanzania ilitambulishwa August mwaka ikiwa na wajumbe wafuatao:
1.Juma Pinto – Mwenyekiti
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi – Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe
Wajumbe wa Sekretariet ni:
1. Dr.Ramesh Shah
2. Hidan Ricco
3. Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni
No comments:
Post a Comment