ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 19, 2016

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI, MEJA JENERALI RWEGASIRA ALITAKA JESHI LA ZIMAMOTO KUONGEZA KASI KUKUSANYA MAPATO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto) akiwasili Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba, kulia ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha. Katika hotuba yake, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kulia) akitoa taarifa ya utendaji wa Jeshi lake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (wapili kulia) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba. Kulia ni Fikiri Salla, Kamishna wa Usalama kwa Umma Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Rogatius Kipali (kushoto)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba (wapili kushoto) akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kulia) wakati Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) alipoambatana na Naibu Katibu Mkuu huyo katika ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam leo. Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu, Meja Jenerali Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Kushoto ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Rogatius Kipali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba (kulia) wakiwa na maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (watatu kulia), wakizungumza jambo mara baada ya Katibu Mkuu huyo kumaliza kulikagua jengo la ghorofa tano la Ofisi za Makao Makuu ya jeshi hilo, lililopo Tazara Mchicha jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, 

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

2 comments:

Anonymous said...

Nchi haijengwi kwa bila sheria au kanuni
Chonde Chonde Magufuli

Anonymous said...

Badala ya kuangalia utoaji huduma nzuri unasisitiza ukusanyaji mapato. Kwani jeshi ni kampuni ya kibiashara au? aibu sana hii

mdau UK