ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 20, 2016

MABONDIA SADIQ MOMBA NA BAINA M,AZOLA WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 TASUBA BAGAMOYO

Mabondia Sadiq Momba kushoto wakitambiana na Baina Mazola baada ya kutia saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa pwani katikati ni promota Muhusin Sharif 
Promota wa mchezo wa masumbwi Muhusin Shsharif katikati akiwa pamoja na mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola mara baada ya mabondia hawo kutiliana saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani 
KIONGOZI KUTOKA KATIKA KAMPUNI YA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA PST PEMBE NDAVA KATIKATI AKISAINI MKATABA WA KUKUBALI KUPIGANA BONDIA BAINA MAZOLA KUSHOTO NA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU
Promota wa masumbwi nchini Muhusini Sharif Katyikati akiwainuwa mikono juu mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola wakati wa kutambulisha mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani 
BONDIA SADIQ MOBA AKITIA SAIN YA KUZIPIGA NA BAINA MAZOLA MARCH 5 KATIKA UKUMBI WA TASUBA BAGAMOYO MKOA WA PWANI WANAOSHUDIA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU NA KIONGOZI KUTOKA NGUMI ZA KULIPWA PST PEMBE NDAVA

Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Sadiq Momba na Baina Mazola jana wamesaini mkataba wa kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo Mkoa wa Pwani uzito kwa kg 59
akizungumza wakati wa kutiliana saini kwa ajili ya mpambano huo promota Muhusini Sharif amesema ameamua kuwapambanisha mabondia hawo wanaotamba kwa sasa kwenye uzito uho kwa ajili ya kuleta chachu ya mchezo wa ngumi nchini

unajua Sadiq Momba ni bondia maarufu ambaye anakwenda sana nje ya nchi kwa ajili ya mapambano mbali mbali na amekuwa anafanya vizuri awapo nje ata hivyo mpambano wake wa mwisho nchini Thailand amepigwa kwa T.K.O ya raundi ya tatu na kurudi nyumbani hivyo anacho itaji ni ushindi na kupigana na mtu mwenye point za kutosha kumrudisha kileleni

na Baina Mazola katika uzito wake yeye ni namba tatu katika boxrec nchini hivyo nae anataka kuwa zaidi ya bondia Momba na ndio anatishia amani katika uzito uho kwa sasa

nae bondia Momba amesema baada ya kupoteza mpambano wake nje ya nchi sasa wadogo zake wanamtaka kucheza nae kwani inaonekana kiwango changu kimepungua na kudiliki watoto wadogo kunitaka mimi ata ivyo nashukuru uhu mchezo mimi ni kazi yangu naitegemea ivyo nitaakikisha simpi nafasi ata chembe kwa kumpiga kipigo kibaya sana ambacho ajawai kupigwa tanga aanze mchezo wa masumbwi nchini

nae bondia Mazola amesema kwa sasa yupo vizuri sana na anawaomba mashabiki zake kuwa na moli ya kwenda bagamoyo ambapo promota kafanya vizuri sana klupereka mpambao huu uko sisi mabondia wote wawili tuna umarufu mkubwa sana maeneo ya manzese na vitongoji vyake ata hivyo nita akikisha nampiga Momba kama begi kwa kuwa sasa ana jipya nimeona stail zake zote anazotumia kupigana sijaona jipya hivyo ajiandae kwa kipigo tu

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments: