Wakili
wa Nemc, Manchele Suguta (kushoto) akizungumza na mawakili wa walalamikaji,
George Mwalali (kulia) na Abubakar Salim mara baada Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, kuweka zuio
la kusitisha ubomoaji wa nyumba zaidi ya 681 za wakazi wa mabondeni jijini Dar
es Salaam.
Wakati shauri lao likiendelea wakazi wa mabondeni wakiwa wametulia kusubiri maamuzi ya mahakama.
Wakati shauri lao likiendelea wakazi wa mabondeni wakiwa wametulia kusubiri maamuzi ya mahakama.
Wakili
wa Nemc, Manchele Heche akizungumza na waandishi wa habari.
Wakili wa wakazi wa mabondeni, Abubakar Salim akizungumza na waandishi wa habari.
Wakazi wa mabondeni waliofungua kesi ya kupinga kubomolewa nyumba zao wakimsikiliza mbunge wao, Maulid Mtulia CUF)
Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF), akizungumza na wakazi wa mabondeni mara baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kutoa uamuzi wa kuweka zuio la ubomoaji wa nyumba 681 za wakazi wa mabondeni.(Picha zote na Francis Dande)
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha
Ardhi imeweka zuio la kubomoa nyumba zilizopo katika wilaya ya Kinondoni hasa
zile ambazo wamiliki wameleta ombi lao mahakamani kuzuia kubomolea.
Akitoa hukumu hiyo mbele ya
walalmikaji Mwanasheria wa Serikali, mawakili wa walalmikaji na wananchi Jaji
wa Mahakama hiyo kuu ya Ardhi Mhe.Panterine Kente amesema kuwa mahakama
imezingatia maelezo toka pande zote mbili na kuangalia madhara watakayopata
wananchi kwa kutekelezwa kwa zoezi hilo.
Jaji Panterine Kente ameongeza kuwa
mahama ya Ardhi haijaweka zuio la bomoa bomoa kwa Tanzania nzima bali kwa wale
tu walioleta maombi ya shauri la zuio la kubomolewa nyumba zao na kusisitiza
kuwa Serikali itaendelea na uwekaji wa
alama za x na ubomoaji wa nyumba zilizopo sehemu hatarishi na sehemu
zisizostahili.
“ Nakuagiza Wakili Abubakari Salim
uniletee majina yote leo hii na sio kesho ya waliofungua shauri la zuio la
kutobomolewa nyumba zao ili tuweze kuendelea na zoezi la ubomoaji” Alisema Jaji
Kente
Akizungumza baada ya kutolewa hukumu
hiyo Wakili wa Serikali Manchare Henche amesema wamepokea hukumu hiyo na
wao wataendelea na majukumu yao ya ubomoaji wa meneo hatarishi kama Mahakama
ilivyoeleza kuwa haijatoa zuio la bomo bomoa kwa Tanzania nzima ila kwa wale tu
walioleta shauri la zuio.
“Tunaomba walio maeneo ya mabondeni
wahame kwani zoezi hili linaendela na zoezi la uwekaji wa alama za x litaendelea
kama kawaida kwa maeneo mengine nje ya haya yaliyowekewa zuio” Alisema Subuta.
Aidha akizungumza na waandishi wa
habari baada ya kutolewa hukumu hiyo Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia
amesema kuwa uamuzi umeridhisha na pia mahakama imetenda haki kwa wananchi wa
kinondoni na wanashukuru kwa kupata nafasi ya kusikilizwa kwa hoja zao.
Kesi hiyo namba 822ilifunguliwa na
wawakilishi nane wanaowawakilisha wanachi 674 ambao nyumba zao zilikuwa katika
mpango wa kubomolewa chini ya sheria za
mipango miji.
Baada ya Mahakama kuu ya Tanzania
kitengo cha Ardhi kutoa zuio la bomoa bomoa kwa wakzi hao kesi ya msingi
itatajwa tena januari 11.
No comments:
Post a Comment