Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na kikosi kazi chake wakiwasili katika jengo la Alosco Tower lililopo Lumumba jijini Dar es Salaam leo.
MWIGIZAJI na mchekeshaji wa nchini Kenya, Eric Omondi amewasili mchana huu jijini Dar leo akiwa na kikosi kazi chake wakiwa tayari kwa 'LIVE SHOW' kesho katika ukumbi wa mikutano wa Marqee uliopo hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa katika pozi na bango la GSM Media leo alipo wasili jijini Dar es Salaam kwaajili ya 'LIVE SHOW' itakayofanyika kesho katika hoteli ya Hyatt katika ukumbi wa Marqee jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji (katikati) na Dj wa mchekeshaji huo, wakiwa katika ofisi cha GSM Media leo mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiteta jambo na Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji leo jijini Dar es Salaam.
Kikosi kazi cha Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi.
Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji akiwakaribisha wanakikosi kazi wa Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi leo mara baada ya kuwasili katika ofisi za GSM Media zilizopo jengo la Alosco Tower Lumumba jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji na Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi wakiwa katika picha na kikosi kazi cha mchekeshaji huyo ambapo 'LIVE SHOW' itakayofanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akipiga picha na wafanyakazi wa GSM Media leo mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Michuzi Media Group(MMG), Ankal Michuzi akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kazi cha Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi jijini Dar es Salaam leo.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akipewa makablasha ya GSM Media na Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment