Sunday, January 24, 2016

Membe: Serikali isicheze na wafanyabiashara

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali iliyopita, Benard Membe amempongeza Rais John Magufuli kwa kasi aliyoanza nayo katika vita dhidi ya ufisadi na kudhibiti mianya ya wakwepa kodi, lakini akamshauri kuwa mwangalifu katika kushughulikia wafanyabiashara.

Membe alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika mapema wiki hii kuhusu, mambo mbalimbali yanayoendelea tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.

Mwanadiplomasia huyo alisema hatua ambazo Rais Magufuli amekuwa akichukua kuwabana wakwepa kodi ni za msingi, lakini lazima alifanye kwa uangalifu mkubwa ili asiwafukuze wawekezaji ambao kimsingi ndiyo wabia wa maendeleo ya taifa.

“Wafanyabiashara ni watu wa ‘kuwahandle’ vizuri na kwa uangalifu mkubwa kwa sababu wao ndiyo gurudumu la maendeleo ya nchi yoyote duniani,” alisema Membe.

“Tunapozungumzia ajira, tunazungumzia wafanyabiashara ambao ndiyo wawekezaji. Sasa ombi langu ni kwamba Serikali isicheze nao.”

Akitumia ishara ya mkono wake wa kulia, Membe alisema: “(Mfanyabiashara) Ni kama ndege ambaye ili uendelee kuwa naye, ni lazima umshikilie hivi, lakini ukiachia vidole ataruka na kwenda kutaga mahali kwingine.”

Alikuwa akijibu swali kuhusu hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali kuwabana wafanyabiashara wakubwa ili walipe kodi. Katika hatua hizo, Serikali ilibaini zaidi ya makontena 11,800 na magari 2,019 yalipitishwa bila ya kulipia ushuru bandarini na kusababisha Serikali ipoteze Sh 48.77 bilioni.

Pia, ilibaini kuwa kampuni zinazomiliki bandari kavu zilisababisha upotevu wa makontena 349 na hivyo kusababisha Serikali kukosa kodi ya Sh80 bilioni. Serikali ilichukua hatua kwa kubadilisha watendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Mapato (TRA), kuwasimamisha kazi baadhi na wengine kufunguliwa kesi mahakamani.

Katika kikao na wafanyabiashara Desemba 3, 2016, Rais Magufuli pia aliagiza wafanyabiashara ambao hawakulipa kodi, wafanye hivyo ndani ya siku saba kuanzia siku hiyo.

“Ingekuwa mimi sikupi siku tatu wala siku saba kulipa kodi. Nakupa miezi miwili mpaka mitatu ili uweke sawa mahesabu yako kwa sababu kutunza hesabu siyo jambo rahisi na baada ya hapo nitakwambia tuendelee kuijenga nchi pamoja,” alisema Membe, ambaye pia aliomba ridhaa ya CCM ili agombee urais, lakini akaishia kwenye tano bora.

Membe, ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka tisa, alisema wafanyabiashara wana masikitiko makubwa dhidi ya Serikali na anaona suala hilo litaibuka bungeni kwa kishindo safari hii kwa kuwa wengi hawaridhiki.

Membe alibainisha kuwa moja ya masikitiko ya wafanyabiashara hao ni kupewa notisi ya muda mfupi kulipa kodi wanazodaiwa kukwepa katika uingizaji wa makontena bandarini.

Agusia kilio cha Lowassa

Membe pia aligusia tuhuma alizotoa aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa kuwa wafanyabiashara waliounga mkono wagombea wa upinzani wananyanyaswa na kuandikiwa kodi kubwa.

“Si dhambi wafanyabiashara kufadhili vyama vya siasa wakati wa uchaguzi. Lakini akishapatikana Rais, Serikali ina wajibu wa kuwakusanya wafanyabiashara wote na kufanya nao kazi ya ujenzi wa Taifa na siyo kuwaburuza,” alisema Membe.

Fukuzafukuza

Kuhusu mwenendo wa kutimua na kusimamisha watumishi wa Serikali walio kwenye maeneo yenye harufu ya ufisadi, Membe alisema, “Ni rahisi kumshughulikia mtu usiyemfahamu, lakini siyo rahisi kumshughulikia unayemfahamu”.

Alifafanua kuwa haitakuwa shida kwa Rais Magufuli kuwashughulikia watendaji aliowakuta serikalini ambao kimsingi hakuwateua, kwa kuwa hawafahamu.

“Kwake kufanya hivyo ni rahisi kwa kuwa pia ni rahisi kuwashughulikia watu usiowajua kuliko watu unaowajua, lakini hebu tuone kama atafanya hivyo pia kwa hao aliowateua mwenyewe,” alisema Membe.
Mwananchi

19 comments:

Anonymous said...

Kitu cha kumshukuru Mungu ni kuwa huyu mzee hayupo madarakani. Inaonyesha viongozi wa awamu iliyopita walivyokuwa wanakwamisha maendeleo ya nchi.Utajengaje nchi na wakwepa kodi we mzee?

Anicetus said...

Sorry Mr. Membe for your griviences: Hapa ni kazi tu. Kila mfanya biashara anajua jukumu lake-socialresponsility ..end of discussion. Dr Maguli is-doctarate in Scoince and his tean a no time for nonsense politics. The country is in no torenace, no nonse and kazi tu model. Mhe Membe everyone undertand your pain, but you have to move on. Life is too precius to waste.

Anonymous said...

HUYU JAMAA SAFARI HII KAKOSA HATA UBUNGE.

SASA ASUBIRI 2020 AATAKAPO KUWA RAIS, MAANA TUTAKUNJWA MAZIWA KWENYE MABOMBA YA MAJI.

Anonymous said...

The issue is not who you know, but the issue is rule of law. Once we have this straight; then, we can talk about fair competition. I am not sure if Membe is aware these two items.

It's during Kikwete administration, of course Membe was part of it - we saw people get away with murders. Ppl were committing crime with impunity. As a country, we can't afford that any more. So, please Bernard, go away.

Anonymous said...

Kwa kweli nashindwa kumuelewa ndugu Membe kwani kama kweli yupo sincerely na huo ushauri wake kwanini asitumie ngazi zinahusika kufikisha ujumbe wake au yeye sie mwanachama wa CCM? Kwa nyazifa alizokwisha zikamata ndani ya CCM si dhani kama angelikuwa na wakati mgumu wa kuwasilisha maoni yake kwa magufuli bila kutumia vyombo vya habari. Na kama ndugu Membe anapata wakati mgumu kuwasiliana na uongozi wa magufuli mpaka mnambidi kufikisha ujumbe wake kwa kutumia vyombo vya habari bssi ajue anamatatizo kwani Magufuli hayupo tayari kujishirikisha na majipu. Na vipi ndugu Membe anaposema serikali isicheze na wafanyabiashara, wakati wafanyabiashara wanacheza na serikali na kuisababishia hasara ya mabilioni kwanini hakusikikana akikemea?

Anonymous said...

Membe anapaswa kukaa kimya pengine itasaidia kuficha udhaifu wake.The more anavyojaribu kutoa matamko ndivyo watu wanavyotambua how empty this person is!

Ramboni said...

Tatizo la viongozi wetu ni umasikini na wanapoonjeshwa madaraka kidogo na kupata fursa ya kuiba na kuanza kenenepeana hapo ndipo panakuwa nongwa. Hali kama hii ikishawafika wanakuwa wabinafsi na wanaanza kuyafumbia macho matatizo yote ya nchi na hivyo kuanza kuwanyonya wananchi kwa kupora au kujichotea mali ya umma ambayo wamekabidhia. Pale wanapoondolewa kwenye nafasi hizi na hivyo uporaji huo kuzibika, viongozi hawa wanachanganyikiwa na kuanza kuropoka ovyo. Haya ndiyo yamemfika Bwana Membe. Tangia Bwana Membe alivyoanza kufungua mdomo wake amekuwa anaongea mambo ya ajabu sana mpaka mtu unashangaa na kujiuliza alipataje cheo cha uwaziri katika wizara muhimu kama ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Ati anatuambia kazi za Waziri wa Mambo ya Nje ni kupishana na wenzake angani kama vile nyumbani kunawaka moto. Mara kubana safari za nje ili kupunguza gharama za serikali zitalifanya taifa letu kutengwa kama kisiwa – Bwana Membe ukumbuke hata wakati wa Rais wa awamu ya kwanza, Hayati Mwalimu Nyerere safari za nje zilikuwa zimedhibitiwa na bila kibali cha Ikulu huwezi kununua tiketi ya ndege wala kupata hela ya kigeni hapo Benki Kuu. Sasa tena anakuja na mpya ati rais asipokuwa mwangalifu anaweza kuwafukuza wafanya biashara kwa ajili amekuwa makini kwa kuwafuatilia wanaokwepa kulipa kodi. Bwana Membe katika tembea yake yote aliyofanya nchi za nje anaweza kutuambia ni nchi gani ambayo inacheza mchezo wa madogoli katika kukusanya kodi! Mimi naishi hapa Marekani na hapa wanakwambia unaweza ukaua mtu na mahakama ikakuachia lakini usipolipa kodi ujue utafungwa, biashara yako pamoja na mali yako itafilisiwa na bado ukitoka jela kodi hiyo utailipa. Swala hili linafanyika kwenye nchi nyingi zenye viongozi wenye uchungu wa maendeleo ya wananchi wao na hivyo wizi, rushwa na ubinafsi hazikubaliki. Ndugu yetu huyu bahati mbaya hakupata alichotaka hivyo akae nyumbani ajitulize na kupanga mikakati ya miaka ijayo badala ya kuropoka maswala ambayo hayana maana kwa Watanzania tunaoipenda nchi yetu na hivyo tunataka maendeleo kwa kila mwananchi. Hao wafanya biashara wanaomfuata kueleza masikitiko yao ya kutozwa kodi awaambie hii ni Tanzania mpya na "hapa ni kazi tu" na kama maandiko muhimu ya kidini yanavyosema "Cha Kaizari, Mpe Kaizari" – hivyo inabidi walipe kodi kama wanataka kufanya biashara nchini. Kama hawataki kulipa, waende kwingine kokote kule ambako kodi haitozwi bahati mbaya mimi sijui ni nchi gani ambayo haidai kodi za aina hii

Anonymous said...

Sasa mtu kama huyu si ndio lile kundi la watu wenye IQ ndogo. Ndio maana hawaishi kutusema mtu mtu mweusi ana IQ ndogo na wanadai wamethibitisha hivyo. Si kutokana na mazezeta wachache kama huyu. Alafu atajisema msomi. Msomi wapi? na IQ yako ndogo

Anonymous said...

Jamani huyu Membe alimaliza masomo ama alinunua hivyo vyeti vyake, akili gani hii ya kujenga uchumi kwa kutolipa kodi na kujuana

Anonymous said...

Anonymous said..,
We know how painful is for a gentlemen to be exposed of its weakness, sorry you need to relax and let the true champion lead the country, it is only a straight talk time not anymore nonsense!!! Bye Bernard!

Anonymous said...

Thanks Mr. Membe, we see what could be your relations with business community however we have difficulties to understand how it is easy for you to relate business community record keeping culture. Do we as Tanzanian keep on our development culture of waiting instead of going to work on that HAPA KAZI moto? These people all have the records of what they have swindled the Nation you think they need months to repay the swindled money? I am sorry they know and they knew whats good then and knew what was bad and wrong then. We(Tanzanians)knew and know what kind of President we would have Elected by electing you. Please take a break from politics and choose your friends and not on Tanzanians back. We are listening and watching.

Anonymous said...

Mdau wa Marekani uliotoa maoni hapo juu nakupa high five, kodi sio kitu cha kuchezea kwa maendeleo ya nchi. Tumesikia mastaa maarufu kama akina Wesley snipes kusotea jela kwa kosa la kutolipa kodi. Au mfanya biashara maarufu, mama aliekuwa akiheshimika kabisa katika vipindi vyake vya biashara kupitia tv Martha Stewart kusotea jela miaka kadhaa kwa kosa la kutolipa kodi. Na wengi wengineo nakadhalika mastaa na wafanyabiashara wakubwa wanejikuta wakisotea jela hapa Marekani kwa kosa la kutolipa kodi ndio maana tunapaona hapa Marekani pazuri lakini uzuri huu tunaouona kama serikali zetu zitaendeshwa na viongozi ya aina ya kina Membe basi tusahau kabisa kufikiria yakuwa nchi yetu inaweza ikafika kokote kimaendeleo.

Anonymous said...

Hivi kumbe huyu Bwana siku zote alikuwa nje ya nchi hata hatukupata kumfahamu. Sasa safari hazipo, shughuli mjini ni Hapa Kazi Tu, na ndio tunapata fursa ya kuwafahamu jamaa wengine!! Inasikitisha kweli. Babu huyu hanamshauri?

Anonymous said...

Membe! Membe please go away!!! Ulipewa cheo kwenye ngazi ya juu ukajisahau!! Sasa unamuonea gere Muheshimiwa Magufuli na team yakeeeeee! Wewe nenda zako hukooooo kapumzikeeee tu! Hatuitaji mawazo yakooooo!

Anonymous said...

Poor Membe is all I can say.

Anonymous said...

KWELI MAGUFULI DESERVES OUR PRAYERS. WABAYA WAKE WENGI HATA NDANI YA CHAMA CHAKE WALIOKOSA FURSA WALIZOKUWA WANAZITUMIA KWA MASLAHI BINAFSI

Anonymous said...

Hatareee

Anonymous said...

Nadhani Membe anayo haki (God's given rights) ya kutoa maoni yake kama Wadau wote hapo juu mlivyofanya kwake. Criticising government leaders is commonplace in the 21th century World, so why should it be an exceptional to Tanzania? Tuache ushabiki wadau, hii ndiyo demokrasia, no matter how unpalatable Membe's comments are! Demokrasia ni mchezo wa kuvutana. Tanzania siyo nchi ya dictatorship, eti so and so can't criticise the government or president? Give me a break folks, especially you, the western educated fellows who knows better!

Ramboni said...

Anony. wa January 27, 2016 nakubaliana nawe kabisa kuwa kwenye nchi inayoendeshwa kwa demokrasia kama nchi yetu kila mmoja wetu ana haki ya kutoa mawazo yake. Ni kwa misingi kama hii ndiyo maana tuko huru kukosoa na kukosoana, siyo sisi raia tu bali hata na viongozi wetu na kwa hili hakuna ushabiki wa aina yoyote. Hivyo Bwana Membe kumkosoa Rais anavyoshughulikia matatizo ya nchi yetu ni haki yake kabisa kwani kwa kufanya hivyo ndiyo njia pekee ya kujadili kasoro ambazo atakuwa ameziona na hivyo kuruhusu wengine kuchangia mawazo yao kwa manufaa ya taifa letu. That said, some of us who contributed to this debate and while appreciating Mr. Membe's comments, have differed with him on the way he thinks corruption, tax evasion and other problems facing our beloved nation should be handled. These problems are serious ones and need to be addressed now and not latter and we are happy that we now have President Dr. Magufuli who is willing to do that. For your information, although we may be western educated and possibly living in western countries but we can assure you that some of us got our education up to first degree level in our home country where I can guarantee you that we got very good education not to be compared with what you may have in your mind.