Saturday, January 16, 2016

'Mgonjwa wa Magufuli' afungwa Muhimbili

Chacha Makenge (39), ambaye ni maarufu kwa jina la ‘mgonjwa wa Magufuli’ ameondolewa wodini kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), jijini Dar es Salaam, na kupelekwa wodi ya magonjwa ya akili kwa nguvu, kwa kutumia amri ya mahakama.

Kuwekwa wodi ya magonjwa kwa amri ya mahakama ni moja ya aina ya hukumu za mhimili huo wa dola.

Zoezi hilo la kumhamisha lilifanyika juzi saa 6.30 mchana ambapo uongozi huo ulimpeleka katika kitengo cha magonjwa ya akili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kutokana na vitendo vyake kutokuwa vya kawaida.

Akizungumza na Nipashe jana, Ofisa Ustawi wa Jamii wa MOI. Frank Matua, alisema walichukua hatua hiyo baada ya Makenge kugoma kuondoka wodini mara kadhaa licha ya kuruhusiwa na madaktari baada ya afya yake kuwa nzuri .

Makenge alilazwa wodi ya Sewahaji namba 18 na kitanda chake kilikuwa cha tatu mstari wa kwanza, upande wa kushoto unapoingia wodini.

Alisema baada ya kuona mgonjwa huyo anaendelea kung’ang’ania wodi na kukaidi maelekezo ya madaktari, waliamua kwenda mahakamani kuomba kibali cha kumuondoa kwa nguvu kwenda kumpima akili.

“Tumemuondoa kwa kutumia amri ya mahakama na kumpeleka kitengo cha magonjwa ya akili, kule ana faili lake la siku nyingi," alisema Mutua na kueleza, "sasa MOI haitawajibika na Makenge kama ilivyokuwa huko nyuma.

"Ametusumbua hapa kwa muda mrefu sana ingawa tumepata shida kumuondoa, lakini tumefanikiwa.”

Alisema Makenge aliwapa changamoto nyingi kwani awali alipopelekwa katika kitengo cha magonjwa ya akili, siku ya pili alitoroka na kurudi Moi.

“Tunaamini mgonjwa wetu alikuwa na matatizo ya akili na ndiyo maana tukachukua hatua ya kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumchunguza,” aliongeza kusema.

Novemba 9 mwaka huu wakati Rais Dk. John Magufuli, alipofanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Muhimbili, alikutana na Makenge ambaye alimwelezea matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo wagonjwa na hasa kuharibika kwa mashine za CT-Scan na MRI.

Rais Magufuli baada ya kupewa taarifa hizo na Mekenge, aliamuru mgonjwa huyo atibiwe kwa gharama zake hali ambayo ilisababisha watu wamwite mgonjwa wa Magufuli.

Mgonjwa huyo amekuwa na vituko vingi tangu awasili hospitalini hapo mwaka jana ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kwenye taasisi hiyo, Samuel Swai, alisema Makenge amekuwa msumbufu kiasi ambacho madaktari wameshauri kufanya utafiti zaidi kuhusu matatizo mengine.

"Sisi madaktari baada ya kumfanyia vipimo vyote na kumtibu ugonjwa uliokuwa ukimsumbua, tumejiridhisha hana tena matatizo yaliyomsumbua nyuma ya mgongo lakini cha ajabu hataki kuondoka," alisema Swai.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa kwa muda mrefu Chacha amekuwa na vituko vingi kwenye wodi aliyolazwa, ikiwa pamoja na kukataa kulala kitandani na badala yake amekuwa akilala chini hali ambayo iliwalazimu kuanza mchakato wa kupima akili yake.
CHANZO: THE GUARDIAN

5 comments:

Anonymous said...

Asante sana kwa taarifa.
Naomba tu kuuliza, hii habari mnashirikisha umma mkiwa kama Madaktari hamtambui kuhusu bridge ya confidentiality. Au kwa sababu ana dalili za ugojwa wa akili? kwani angekuwa mzazi wenu mngeleta huku kututangazia.

Pengine tunaweza kuwasaidiaje endapo mmepleleka kupima akili ? Na kwani ugojwa wa akili si ugojwa kaka magojwa mengine..... Nyie ndio mnatakiwa kusaidia taifa katika fight agaist stigma and not otherwise.
Naomba mheshimu utu wa mtu na msi-violate code of conducts.
We as patients have entrusted you to make correct judgment on our health weather we are physically ill, mentally ill, or unconscious. That is why we give you the respect and you have got to reciprocate same respect to those who have entrusted you with their live especially at the most vulnerable times of their lives.This is a very private matter and not for public display and humiliation. What should his family feel? Shame on you and take our excellence Dr. Magufuli name out of this, we are here for serious matters.

Anonymous said...

Like x 3

Anonymous said...

Annon hapo juu. I agree that they should practice patient confidentiality. Yes he is a patient like anyone one else so respect and confidentiality should be practiced. Laws should be passed on people, health care workers who violate patients rights, information and pay a big fine .e.t.c

Anonymous said...

Hawana lolote kwa kuwa kasema ukweli. Na kuwaumbua basi imekuwa tabu, mijitu myeusi bwana haishi roho mbaya. Siku hadi siku, inapenda utajiri bila kutolea jasho ndio maana kutwa kuuwa wenzao. Mfano albino.inapenda wizi,ufisadi, mataifa ni maskini kwa kwenda mbele yote Miroho ya mdaraka ili iibe, umasikini umejaa kila kona, haina hata huruma na wenzao.

davidmusika said...

Mgonjwa kapoteza sifa kwa sababu amekuwa involuntary patient na sio voluntary patient. Na kwa vile kesi imeamuliwa mahakamani huwezi kulinda haki za mgonjwa kujulikana ingawa HIPPAA ni lazima kwa kila mgonjwa