Saturday, January 16, 2016

MISA YA KUMBUKUMBU YA MPENDWA MAMA YETU LETICIA NYERERE KUFANYIKA LEO JUMAMOSI ST EDWARD, BALTIMORE

Leticia Nyerere enzi ya uhai wake

Familia ya Nyerere inependa kuwataarifu, kuwakaribisha na hatimae kujumuika nao katika misa ya kumbukumbu ya mpendwa mama yao Leticia Nyerere itakayofanyika leo Jumamosi Januari 16, 2016 saa 6 kamili mchana (12 pm sharp) katika kanisa la Mtakatifu Edward lililopo Baltimore, Maryland kwenye anuani ifuatayo hapo chini.
 901 Poplar Grove Street,
Baltimore, MD 21216

Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio.

 Kwa maelezo na maelekezo zaidi tafadhali wasiliana na 
Margareth Mageni 240 462 9138
Emmanuel Muganda 240 447 2801
Ramadhani Kamguna 202 459 3839

Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.

Mheshimiwa Wilson Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani akiweka sign kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Laticia Nyerere Lanham. MD. U.S.A. Kwa taswira zaidi za nyumbani kwa marehemu nenda soma zaidi.


Kada wa CCM Washington, DC Salma akiweka sign kwenye kitabu cha maombolezo.


Kushoto Mume wa Marehemu Laticia Nyerere Bwana Madaraka Nyerere akiwa nyumbani hapo.
Watoto wa Marehemu Julia Nyerere.


Ni mtoto wa marehemu Laticia Nyerere anaitwa,  Helena Nyerere.


Colonel Adolph Mutta Defense Attaché. alikuwepo pia nyumbani kwa marehemu kutoa pole.

Mr Suleiman Saleh Minister Plenipotentiary, Political Affairs alikuwepo pia. 


Marafiki wa familia ya marehemu wakiwa nyumbani kutoa pole.
Dr Temba, wa Temba Engineering Services kutoka Brooklyn, New York katikati akiwa nyumbani kwa wafiwa.




6 comments:

Anonymous said...

Pumzika kwa amani dada Leti.

Anonymous said...

Bwana ametoa na bwana ametwaa,Jina la bwana libarikiwe

Anonymous said...

Mungu ampumzishe kwa amani

Anonymous said...

Mungu amempenda zaidi akamchukua. R.i.p. dada leti.

Anonymous said...

Dadangu umeniuma sana. Umerutoka kama utani jamani! Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi. Rest in peace my sister! Amen

Anonymous said...

poleni sana wafiwa wote na watoto wa marehemu na ndugu na jamaa wote mungu akupeni nguvu na moyo wa subra.
ni njia yetu sote tutakwenda huko.sema tunasubiri tu saa na wakati wetu ukitimia tutakuwa naye mpendwa wetu amen.

na ibra NY umependeza sana bro.samahani lakini wafiwa.kwa kauli yangu hii.