ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 5, 2016

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA UHAMIAJI, AAGIZA MAKAMPUNI YENYE KUAJIRI WAGENI YACHUNGUZWE

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Masauni aliiagiza Idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini.. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (kulia) akiwasalimia wananchi wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake kwa Viongozi Wakuu wa Idara hiyo, Naibu Waziri Masauni aliiagiza Idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini.
Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa Hati za Kusafiria, Amir Hassan (kushoto), akitoa maelezo ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria, kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati aliyevaa tai) ambaye alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao chake na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile, na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja.
Kamishna wa Idara ya Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja akitoa taarifa fupi ya utendaji wa Idara hiyo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati) wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (wanne kushoto), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji. Naibu Waziri Masauni alifanya ziara ya kikazi katika idara hiyo kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na idara hiyo. Hata hivyo, katika hotuba yake, aliiagiza idara hiyo kuchunguza Makapuni yanayotoa ajira kwa wageni ambapo ajira hizo wangepewa Watanzania wenye sifa na kupunguza tatizo la ajira nchini .

3 comments:

msema kweli said...

Jamani watanzania tuache UJINGA, UPUMBAVU NA UKICHAA wa kuwapa ajira na kuwanyima fursa watanzania ambao wapo na sifa za kutosha.Hii biashara ya kuleta wachina kujenga barabara ni ushenzi mkubwa.Ina maana ma- engineers wa Tanzania hawawez kujenga barabara?hii ni aibu tunafanya na hata dunia inatushangaa.Jaman watu tunaoishi ughaibuni tuko na masters degree na wengine Phds(degree ya uzamili na uzamivu)na experience za kutosha, hupewi kazi hadi kuwe hakuna Mzawa aliye apply. Na kwa sisi waafrika km unaishi Norway watahakikisha ajira hiyo anapewa mzungu kwanza kutoka nchi zozote 14-za Ulaya. Sasa ndio ufikiriwe wewe Mwafrika.Sasa imagine ili upate hiyo kazi basi hapakuwepo M-norwegian, m-sweedish,m-finland, m-germany hakuna m-romania, m-spain, m-holanz, hakuna m-switzerland aliyeomba hiyo kazi,ndio wewe kibirit ngoja utapata hiyo nafasi. This is good,I can't complain, kwakuwa ndivo inavyopaswa kuwa.Sasa ukimbagua mwenyeji,ukamthamin mgeni huyu mwenyejiakaajiriwe wapi?. NARUDIA MNAOFANYA HIVO ACHEN MARA MOJA, MAANA NI UJINGA ULIOPITILIZA.Mzawa kwanza 2016.

Anonymous said...

Kama ni kweli ulichoandika, hayo mambo ya Ulaya yana chembechembe za kibaguzi. Inaelekea hapo discrimination by origin ndicho kinachoendelea, which is quite wrong! Kama wewe una asili ya Africa lakini unaishi Norway kihalali na una kibali cha kufanya kazi, hupaswi kufanyiwa huo ubaguzi. Kama ni mhamiaji haramu kimsingi husitahili kuajiriwa na yeyote!

Anonymous said...

Anachoongea jamaa yangu hapo juu ni sahihi it is happening. So we need to be patriotic as well.lazima tuajiri watanzania wenye uwezo kufanya kazi ktk projects zetu