Thursday, January 7, 2016

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU





JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na kumtakia heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.Jaji Warioba ameongeza kuwa Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali ya umma.
"Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo" alisisitiza Jaji Warioba.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam.
07 Januari, 2016

3 comments:

Anonymous said...

Jamaniiii ningependa hawa Marais wastaafu wasikanyage Ikulu sababu watamfundisha Muheshimiwa Magufuli mabaya Yao waliyoyafanya hadi kuweka nchi katika Hali mboovu iliyopo au aliyoirithi mh. Magufuli!!!! Wanaenda enda Ikulu kutafuta niniiiiiii? Juzi Kikwete alikuwepo, Leo Mkapa , kunaniniiiiii???? Muh. Magufuli Tanzania inakuombea sanaaaaa, wembe ni huyo huo hakuna kuangalia kushoto, kulia, wala kuyumba ni mbele kwa mbeleeee Tu!!!

Anonymous said...

all these former leaders, are they scared na speed ya Magufuli?

I think hawa wote ni chanzo ya matatizo yaliyopo. They didn't care because they were part of the greater system.

These are the ones who should be locked first. Haya ndiyo mapapa, we are dealing na dagaa.

Anonymous said...

I disagree with the above two commentaries, @7:38P and 9:14P respectively. JPM is the by-product of President Mkapa. Give credit to his excellence former president Mkapa for breaking the impasse during the CCM nomination process, that brought JPM candidacy to fruition. Equally significant, JPM was one of the early cabinet members in the Mkapa administration and that, includes JPM's current chief secretary Mr. Sefue. While they may differ in their leadership styles, both men are known to be workaholics. I thoroughly recall the 90's, when Prez. Mkapa transformed and stabilized Tanzania's economy from almost bankruptcy. I would encourage prez. JPM to entertain positive inputs from these former respected leaders. Contrary to some distractors views, it won't hurt our beloved Tanzania, and frankly, it is the right thing to do.