ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 19, 2016

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MWENYEKITI WA CCM TAWI LA DMV MAREKANI

Napenda kuchukua fursa hii kutuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha ghafla cha mwenyekiti wa Tawi la CCM DMV ndugu George Sebo kilichotokea tarehe 18 Januari 2016, Jumatatu asubuhi katika Hospitali ya Prince George Maryland, nchini Marekani. Kwa kweli kifo hiki cha ghafla tumekipokea kwa mshtuko mkubwa na majonzi Watanzania wote tunaoishi hapa Marekani, kwani George Sebo alikuwa ni mtu mkarimu kwa watu wote bila kujali tofauti zozote za kiitikadi. Nachukua fursa hii kwa niaba ya Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tawi la Washington DC Kumpa pole mke wa Marehemu mama Grace Mgaza, Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na wanachama wote wa CCM kwa msiba huu mkubwa.

Tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu cha Maombolezo.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu GEORGE SEBO Mahali pema Peponi, AMIN.

Mwenyekiti wa Chadema DMV
Kalley Pandukizi

No comments: